Mchezo wa uliochezwa katika dimba la uwanja wa taifa baina ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting umeisha kwa matokeo ya 3-2.
Alikuwa yule yule bwana Amis Tambwe ambaye alianza kufungua kitabu
cha mabao kwa upande wa Simba mwanzoni mwa kipindi cha kwanza kabla ya
kuongeza la pili mwishoni mwa kipindi cha pili. Mpaka mpira unaenda
mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao mawili kwa nunge.
Kipindi cha Ruvu Shooting walirudi kwa kasi na kufanikiwa kupata bao
katika dakika 70, dakika mbili baadae Haruna Chanongo akaongeza bao la 3
kwa Simba. Dakika ya 83 Ruvu wakafunga bao la pili kwa penati baada ya
beki Joseph Owino kuunawa mpira kwenye boksi la penati. Ruvu waliendelea
kulisakama lango la Simba lakini bahati haikuwa yao na mpaka refa
anapuliza kipenga cha mwisho matokeo yalikuwa 3-2 – Simba wakitoka na
ushindi.
0 comments:
Post a Comment