Sunday, 2 March 2014

SOKA WACHEZE YANGA VS AL-AHLY VITI WANG'OE SIMBA? "HAYA MAMBO HAYAELEWEKI"

 



Jana  katika Mchezo wa soka wa kinyang'anyiro cha klabu bingwa Barani Afrika, uliozikutanisha timu za Yanga (Tanzania) na Al-Alhly (Misri) Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam (Tanzania), timu ya Yanga imepata ushindi wa goli moja.

Lakini cha kustajaabisha ni ripoti kuwa kabla hata ya kuanza kwa mtanange huo, baadhi ya mashabiki wa timu ya soka ya Simba ambayo ni wapinzani wa jadi wa Yanga, walianza kung'oa viti na kuvirusha upande walipokuwa wameketi washabiki wa Yanga. 

Chokochoko  hizo inaripotiwa kuwa zilitulia wakati mchezo ukiendelea, ila zikarejea tena mara baada ya Yanga kupata goli, saari hii ni mashabiki wa Simba tena waliovalia jezi za Simba walianza tena kung'oa viti na kuwarushia mashabiki wa timu ya Yanga waliokuwa wakishangilia. Tizama picha zaidi hapo chini...







Kikosi cha Yanga:- Deogratias Munishi, Nadir Haroub 'Canavaro', Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi, Mrisho Ngassa na Hamis Kiiza.

(Aiba: Juma Kaseja, Juma Abdul, Athuman Idd 'Chuji', David Luhende, Hassan Dilunga, Didier Kavumbagu na Said Bahanuzi.)

Kikosi cha Al-Ahly: Sherif Ahmed, Saadeldin Saad (c), Mohamed El Ghareeb, Ahmed El Moneim, Sayed Wahed, Shihab Saad, Hossam Mohamed, Ramy Abdel Aziz, Moussa Yedan, Mohamed Ismail na Amr Sayed.


(Akiba: Ahmed Gamal Mo, Amed Ahmed, Wael Kamel, Elsayed Mahdy, Mahmoud Ibrahim, Ahmed Adam na Ahmed Abdelraouf.)

Related Posts:

0 comments: