Taarifa
 iliyosambaa kwenye mitandao mbalimbali inasema kuwa kuna kundi la watu 
waliokuwa na visu limewashambulia na kuua watu 28 huku zaidi ya 
100 wakijeruhiwa katika kituo cha treni kilichopo mjini Kunming nchini 
China.
Mashahidi
 wa tukio hilo wamesema kuwa washambuliaji hao walivalia nguo nyeusi na 
kuwavamia abiria waliokuwa wakingojea treni na kuwakatakata huku wengine
 wakiwadunga visu wale hasa walioshindwa kukimbia kwa kasi.
Polisi
 wamefanikiwa kuwauwa washambuliaji watano kati ya kumi waliofanya 
shambulio hilo,Shirika la habari la Xhinua limewalaumu watu wanaopigania
 kujitenga katika mkoa wa Shinjiang kwa tukio hilo,ulinzi bado 
umeimarishwa eneo la tukio.
 






 
 
 
 






0 comments:
Post a Comment