Kwa
mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo bwana Fred Mushi amesema kuwa gari aina
ya Landcruiser VX iligonga daladala hiyo iliyo kuwa imesimama kupakia
abiria kwenye kituo kimoja maarufu kwa jina la Kona. Ajali hiyo imetokea
muda wa saa 10.30 jana jioni.
Gari
aina ya Landcruiser VX iliyokuwa na wanafunzi toka chuo cha Mweka ikiwa
imezama kwenye mtaro na kuharibika vibaya baada ya ajali hiyo mbaya
iliyotokea jana jioni.
Pichani
ni mashuhuda walikokuwa eneo la tukio wakilitazama gari aina ya
landcuriser iliyokuwa imezama kwenye mtaro baada ya ajali hiyo
iliyotokea na kusababisha majeruhi.
Daladala
iliyogongwa vibaya na Landcuriser ikiwa imeharibika vibaya ubavuni
kiasi cha kutoweza kutembea tena lakini Taarifa za awali hali ya dereva
wake inasemekana kuwa mbaya pia idadi ya majeruhi mpaka tunaenda
mitamboni haijajulikana.tutaendelea kukujuza jinsi taarifa
zitakavyofikia kuhusu hali na idadi Ya majeruhi.PICHA NA HABARI NA mdau
WITO MSAFIRI WA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG
0 comments:
Post a Comment