Brazil wameahidi shirikisho la
soka duniani FIFA kuwawataimarisha usalama katika viwanja vya kombe la
dunia baada ya tukio ambalo mashabiki wa Chile walikamatwa wakijaribu
kupenyeza ndani ya uwanja bila ya kulipia tiketi ilikushuhudia mechi
baina ya Chile na Uhispania.
Hata hivyo ilikuwa dhiki wa dhiki kwao kwani walipenyeza na kuingia kwa sehemu iliyofungwa kwa ajili ya wanahabari.Idadi ya maafisa wa Usalama watakaokuwa wakishika doria imeongezeka maradufu kutoka kwa maafisa 600 hadi 3,100.
Mashabiki kadha pia wanaripotiwa kuruka uwa wa uwanja wa Beforelast ilikushuhudia mechi baina ya Argentina na Bosnia-Hercegovina.
Katibu wa FIFA anayeshughulikia maswala ya usalama , Ralf Mutschke, alikiri kuwa FIFA ilihuzunishwa na tukio hilo na kuwa itafanya kila iwezalo kuzuia aibu kama hiyo kurejelewa tena katika mechi zote zilizosalia.
0 comments:
Post a Comment