MANCHESTER United imewafunga mabingwa wa Ulaya, Real Madrid mabao 3-1 katika Kombe la Kimataifa Uwanja wa Michigan mjini Ann Arbor, Detroit nchini Marekani.
Shujaa wa United alikuwa ni winga Ashley Young aliyefunga mabao mawili- huku bao pekee la Real likifungwa Gareth Bale.
Young alifunga bao la kwanza kwa kikosi cha Louis van Gaal dakika ya 20, kabla ya Madrid kusawazisha kwa penalti kupitia kwa Bale dakikan ya 27.
Lakini Young tena akamuinua kitini kocha Van Gaal dakika ya 37 akiunganisha vizuri krosi kumtungua kipa Iker Casillas. Nyota wa zamani wa United, Cristiano Ranaldo ambaye kabla ya mcheo huo alisema hajawahi kukataa kurudi timu hiyo, aliingia dakika ya 74, lakini akashindwa kuisaidia timu yake.
Umati wa mashabiki 109,00 ndani ya Michigan mjini Ann Arbor
Gareth Bale akimtoka Michael Keane
Rooney aling'ara jana mjini Detroit
Danny Welbeck akipambana na beki 'mtata' Pepe
Ronaldo alishindwa kuiepusha na kipigo Real jana
Shaw na Tyler Blackett wakitafuta mbinu za kumpokonya mpira Ronaldo
Javier Hernandez ‘Chicharito’ akawafungia Mashetani Wekundu bao la tatu dakika ya 80 mbele ya mashabiki 109,318 waliotapisha Uwanja wa Michigan.
Kikosi cha United kilikuwa; De Gea, Keane, Jones, Evans/Blackett dk45, Valencia/Lingard dk61, Herrera/Cleverley dk45, Fletcher, Young/Shaw dk45, Mata/Kagawa dk61, Welbeck/Zaha dk41 na Rooney/Hernandez dk61.
Real Madrid; Casillas, Arbeloa/Ronaldo dk73, Pepe, Ramos, Fernandez, Alonso/De Tomas dk55, Carvajal, Illarramend, Modric, Bale na Isco.
0 comments:
Post a Comment