Wednesday 21 May 2014

MPIRA PESA WASEMA WAZI KUWA RAIS WAO NI HUYU HAPA




Tawi la wanachama wa Wekundu wa Msimbazi la Mpira Pesa lililopo Jijini Dar, limetoa tamko kwamba  watamchagua Evance Aveva kuwa rais wao katika kipindi kijacho cha uongozi wa timu hiyo.

Awali tawi hilo lilizungumza kwamba kama Hassan Dalali angechukua fomu ndiye wangempigia kura ili awe rais wa timu hiyo lakini Dalali hakuchukua fomu na badala yake akamsapoti Aveva.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Ustadh Masoud, amesema baada ya Dalali kutochukua fomu ya kugombea sasa wamegeukia upande wa Aveva ambaye amefanya mambo makubwa kwenye timu hiyo kwa kipindi cha nyuma na hata Dalali mwenyewe anamuunga mkono.
“Sisi kama tawi tumeona tumpe kura zetu Aveva ambaye anaonekana atakuja kuleta maendeleo katika klabu yetu na kingine hata mgombea wetu tuliyempendekeza achukue fomu, Hassan Dalali, naye anamuunga mkono kwa hiyo hakuna sababu ya sisi kumpinga,” alisema Ustadh.
SOURCE: CHAMPIONI

0 comments: