Wednesday 21 May 2014

HANDENI TANGA YATANGAZA KUTOOMBA CHAKULA MSIMU UJAO

HANDENI NA MAENDELEO YA KILIMO NA UFUGAJI

GU4A0761 MMoja ya wakulima wa Mahindi Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Adalbertus Bubelwa wa pili kutoka kushoto akimwelezea Mkuu wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, jinsi alivyoandaa shamba lake. Mkuu huyo wa wilaya alikuwa katika ziara ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali wilayani humo kuangalia mazao mashambani. GU4A1133  
Mkuu wa wilaya ya Handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, kushoto ambaye ni mwenye shamba akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Kilimo wa Wilaya hiyo Bw. Yibarik Chiza, aliyemtembelea Mkuu huyo wa wilaya shambani kwake GU4A1053 Afisa Kilimo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, kulia akiwaelekeza jambo wakulima wa zao la ufuta wa Kijiji cha Misima wilayani humo.  GU4A1457 Mkuu wa wilaya ya handeni Bw. Muhingo Rweyemamu, akisalimiana na mmoja wa wananchi alipotembelea katika kijiji cha Kang’anta kuangalia maendeleo ya mdada wa mifugo na mazao ya chakula na biashara. GU4A1303  
Mmoja wa wakulima wa nanasi wilayani Handeni Bi Sabrina Rory Sasumua, akionyesha aina ya nanasi lenye uzito wa kilo mbini na nusu kutoka katika shambani lake eneo la Kwamsisi wilayani Handeni. GU4A1508 
Baadhi ya akina mama wa eneo la Soni katika wilaya ya Lushoto mkoani Tanga wakifanya biashara za matunda na mbogamboga. 
GU4A0898 

Na Mohammed Mhina, Handeni. WILAYA ya Handeni mkoani Tanga imetangaza kuwa haitaomba tena chakula cha mtaada kutoka serikali kuu kwa msimu ujao kutokana na matarajio ya kuvuna kiasi kingi cha mazao yakiwemo mahindi na ufuta ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita. Mkuu wa wilaya ya Hendeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ya kumtaka kila mwananchi kulima kwa bidii na kupanda kwa kufuata maelekezo ya wataalam. Akiwa katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Manga, Kwamsisi, Kang’anta, Madebe, Misima, Sindeni, Mzeri na Mbagwi wilatyani Handeni, Mkuu huyo wa wilaya Bw. Rweyemamu alisema katika msimu ijao, wilaya hiyo haitaomba tena chakula cha msaada kwa vile wana uhakika wa kuvuna chakula cha kutosha. Amesema pamoja na kwamba mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote zimekuwa zikileta madhara kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa wilaya ya Handeni mvua hizo zimeleta neema na faraja kwa wakulima kutokana na kuimarika kwa mazao yao mashambani. Bw. Rweyemamu  amesema karibu ya maeneo mengi wilayani humo, wamepata mavuno ya kutosha hasa mahindi na ufuta. Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, amesema kuwa wakulima wengi katika wilaya hiyo wamelima kwa kutumia trekta na majembe ya kukokotwa kwa wanyamakazi jambo ambalo amesema litawaongezea ufanisi mkubwa msimu huu. Na kwa upande wao baadhi ya wakul;ima wilayani humo wamesema chakula kitakachopatikana msimu huu wilayani humo hakijawahi kupatikana zaidi ya miaka 30 iliyopita.
Shamba la mahindi katika kijiji cha Manga likionekana kustawi vya kutosha.
 (Picha Zote na Mohammed Mhina)

0 comments: