Sunday 25 May 2014

RAIA NCHUNI UKRAINE WASHRIKI KATIKA UCHAGUZI WA RAIS

 
016339700_40100_0e769.jpg
Taifa la Ukraine hii leo linashiriki katika shughuli ya uchaguzi wa urais uliotajwa kuwa muhimu katika historia ya taifa hilo.
Wagombea 18 wanawania wadhfa huo katika raundi ya kwanza ambayo inajiri wakati ambapo vikosi vya serikali vinakabiliana na wanamgambo wanaounga mkono Urusi mashariki mwa taifa hilo.
Iwapo hakuna mgombea atakayejipatia asilimia 50 ya kura hizo ,raundi ya pili ya uchaguzi huo itafanyika katika kipindi cha wiki mbili zijazo.
Mshindi atakabiliwa na jukumu kuu la kujaribu kuliunganisha taifa hilo mbali na kumaliza ghasia ambazo zimesababisha vifo vya watu 20 katika siku chache zilizopita.

0 comments: