Saturday 24 May 2014

BANDA AAGIZA KURA KUTOHESABIWA NCHINI MALAWI BAADA YA YEYE KUSHINWA

 
140519091536 malawi elex candidate 304x171 bbc nocredit 138d1

Rais Joyce Banda wa Malawi ameamuru kusitishwa mara moja kwa shughuli ya kuhesabu kura na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo ulifanyika jumanne iliyopita.
Akizungumza Ikulu mjini Lilongwe muda mfupi uliopita ameiamuru Tume ya uchanguzi MEC kusitisha shughuli hiyo na kutangaza kuwa uchaguzi urudiwe ndani ya siku 90 kutoka leo na kwamba yeye hatogombea tena urais wa nchi hiyo.
Mwandishi wa BBC Baruan Muhuza amearifu kutoka mjini Lilongwe kuwa Dr Banda amesema amelazimika kuchukua hatua hiyo kutokana na kile alichokiita kuvurugwa kwa mtiririko mzima wa shughuli za upigaji kura,kuhesabu na hata namna ya kusimamia utoaji wa matokeo yake.

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi ya Malawi Jaji Mackson Mbendera amesema kuwa anawasiliana na mwanasheria mkuu wa serikali ili kuangalia uwezekano wa amri hiyo ya Rais kutekelezwa na kama haijavunja sheria ya nchi.
Ila kwa muaonekano wa uchaguzi na kulingana na matokeo ya  awali kwa baaadhi ya vituo nchini humo raisi wa sasa joyce banda  alioneka ameshindwa  na wapizani wake,wadau mbalimbali wasiasa nchin malawi wamedai kuwa labda  joyce banda ameona ameshindwa ndio maana ameona wastishe kuhesabu kula na zirudiwetena ndani ya siku tisini
CHANZO BBC

0 comments: