Friday 23 May 2014

LUIS SUAREZ APASULIWA GOTI,

YAELEZWA ATAPONA MAPEMA NA KUWAHI KOMBE LA DUNIA

RATIBA YA URUGUAY

Juni 14: Vs Costa Rica, Saa 2:00 Usiku, Uwanja wa Castelao
Juni 19: Vs England, Saa 2:00 Usiku, Uwanja wa Sao Paulo
Juni 24: Vs Italia, Saa 11:00 Jioni, Uwanja wa Das Dunas
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amefanyiwa upasuaji wa goti  na anatarajiwa kupona ndani ya muds na kucheza Fainali za Kombe la Duni, amesema mama yake. 
Sandra Diaz amesema upasuaji umefanyika kwa mafanikio na mwanawe anatarajiwa kupona ndani ya wiki tatu, ambayo inamaanisha atauwahi mchezo dhidi ya England Juni 19, mwaka huu.  
Mambo yameenda vizuri: Luis Suarez amefanyiwa upasuaji leo na anaweza kuziwahi Fainali za Kombe la Dunia kuanzia mchezo dhidi ya England

"Upasuaji umemalizika na tunamshukuru Mungu kila kitu kimekwenda vizuri. Matatizo yaliyokuwa yanamsumbua Luis hayakuwa makubwa sana ," alisema kuzungumzia majeruhi ya mwanawe.
Uruguay, ambayo imedai Suarez alipata maumivu hayo katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya England msimu huu, bado inajiamini atacheza Juni 19
BIN ZUBEIRY inafahamu kwamba maofisa wa soka wa nchi hiyo wanaamini mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anaweza kuwa fiti hata wakati wa mchezo wa ufunguzi dhidi ya Costa Rica, lakini ataanza kucheza siku tano baadaye. 

0 comments: