Friday 30 May 2014

FRANK LAMPARD AJIANDAA KUSTAAFU SOKA,




 Lampard prepared for retirement
Imechapishwa Mei 30, 2014,saa 10:19 jioni

FRANK James Lampard amekiri kuwa kwasasa anajiandaa kustaafu kutokana na hatima yake ya baadaye katika klabu ya Chelsea kuwa matatani.
Nyota huyo mwenye miaka 35 mkataba wake uko mwishoni kabisa na tayari ameshawekwa katika orodha wa wachezaji wanaotoswa na Chelsea kuelekea msimu ujao akiwemo Ashley Cole na Samuel Eto`o.
Wakati haijulikana kama atapewa mkataba mpya, kiungo huyo wa kimataifa wa England anahusishwa kuungana na Harry Redknapp katika klabu ya QPR.
Hata hivyo Lampard alipoulizwa kama anaweza kustaafu baada ya fainali zijazo za kombe la dunia, alidai wala hatajutia maamuzi yake ya kuachana na soka.
“Sijui kama nitakuwepo Chelsea msimu ujao. Napenda kuongeza miaka miwili au mitatu, lakini itakuwa nzuri kustaafu nikiwa kwenye kiwango cha juu”.
“Kwahiyo hata ikiwa kesho, sitajutia maamuzi hayo”. Alisema Lampard.

0 comments: