Shamba la vitunguu
Msimamizi
wa shamba la vitunguu la mwekezaji, Onesmo Kihaga ambaye pia ni
mtaalamu wa kilimo cha umwagiliaji kisichotumia mashine akionyesha bomba
linalosafisha maji kutoka bwawani kwenda shambani.
Chanzo cha maji kabla yakuchepushwa.
Bwawa la maji
Mto Mlaga ukiwa umekauka baada ya mkondo wake kuchepushwa na mwekezaji.
Na Mathias Canal
Wananchi
wa Kijiji cha Kitelewasi Kata ya Ilole wilayani KILOLO mkoani Iringa
wameulalamikia uongozi wa kijiji hicho kwa kubinafsisha mto wa maji na
kusababisha umasikini kwa wananchi wa kijiji hicho. (FS)
Wakizungumza
na MjengwaBlog kijijini hapo, wanakijiji hao wamesema kuwa uongozi wa
kijiji umewasaliti wananchi kwa kubinafsisha mto ambao ndio kitega
uchumi cha maendeleo ya kijiji hicho, kwani mmiliki wa mto huo
amewakataza wananchi kufanya shughuli zozote katika eneo la mto huo.
Kijiji
cha Kitelewasi kipo umbali wa kilomita 25 kutoka Iringa mjini ambapo
ndipo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Isaya Kivike mkazi wa Iringa
mjini anamiliki mto Mlaga ambao ulikuwa tegemezi kwa wanakijiji wa
Kitelewasi na vijiji vya jirani kikiwemo kijiji cha Mlolo.
Mto huo
umechepushwa sehemu mbili ya kwanza ikiwa ni kuelekea kwa mmiliki wa
shamba la nyanya kijijini hapo BW FREDRICK MGATA ambaye ni mkazi wa
kijiji hicho na amebeba tuhuma kutoka kwa wanakijiji kuhusu uanzishaji
wa kuuza maeneo ya serikali akiwa kama kivuli cha umiliki wa mashamba
hayo.
ISAYA
KIVIKE ambaye ndiye mmiliki mkuu wa mto huo yeye amezuia maji hayo
kutoka katika maporomoko ya mlima uliopo kijijini hapo kwa kujenga bwawa
ambalo maji yote yaliyotakiwa kusafiri kwenda mtoni yanaingia kwenye
bwawa hilo.
Bwawa
hilo lina urefu wa mita 9 kwenda chini, lakini maji yaliyopo hivi sasa
bwawani hapo yana ujazo wa mita 7.5, maji ambayo huelekea kwenye shamba
la vitunguu ambalo lina ukubwa wa hekari 15, lakini sehemu ya shamba
yenye vitunguu kwa hivi sasa ni hekari 3.5.
kijana wa
makamo ambaye hakutaka kujitambulisha, yeye alitoa tuhuma kwa FREDRICK
MGATA mmiliki wa shamba la nyanya ambaye amesababisha uuzaji wa maeneo
kijijini hapo kwa kujifanya kama ndiye mmiliki wa mashamba hayo kitendo
ambacho wanakijiji hao wamesema kuwa hayakuwa mashamba yake bali
mashamba ya serikali.
STAN
MGATA mwenyekiti wa kijiji jirani cha MLOLO ambaye ni mzaliwa na
mwenyeji wa kijiji cha Kitelewasi yeye amesema kuwa kero kubwa ni kuhusu
eneo lililouzwa na uongozi wa kijiji hicho takribani hekari 17, huku
akisema ameshindwa kutambua haki ya wananchi mahali ilipo.
Mjumbe wa
halmashauri ya kijiji MIKIDADI NGONGANGE wamewahi kumtupia lawama
aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kololo wakati huo Dkt. Mfutakamba ambaye
alilitupa swala hilo kwa afisa ardhi wa wilaya ya Kilolo.
Aidha
NGONGANGE aliitaja mito iliyopo kijijini hapo ikiwa ni pamoja na mto
Kilofi, Mlaga, na mto Ng'ezi ambapo nwenyekiti alikataa kwa kutaka mto k
Kilofi ndio mto unaotoa maji mengi hivyo hakuna haja ya kutaka mto Mlaga.
Hata
hivyo mwenyekiti wa kijiji cha Kitelewasi ULEDI NDENGA yeye alisema
umiliki wa mto huo umefuata taratibu zote za kisheria kuanzia ngazi ya
kijiji, kata, wilaya na hatimaye kupewa kibali na ofisi ya bonde la mto
Rufiji (Rufiji Basin).
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Ilole JOHN MPONDA amekiri kuwa ISAYA
KIVIKE anamiliki mto huo lakini anamiliki kihalali kutokana na
makubaliano kati yake na serikali ya kijiji japo amekiri kupokea
malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya ubinafsishaji wa mto huo.
0 comments:
Post a Comment