Friday 23 May 2014

CECAFA NILE BASIN CUP: PAZIA KUFUNGULIWA LEO

KWA VICTORIA UNIVERSITY KUVAANA NA MALAKIA FC, MBEYA CITY FC KUWASILI KHARTOUM MCHANA

SC-Victoria
Victoria University wanaanza kampeni yao leo
Na Baraka Mpenja wa  , Dar es salaam
MICHUANO mipya ya CECAFA Nile Basin Cup inatarajia kuanza kutimua vumbi nchini Sudan leo ijumaa kwa mechi tatu kupigwa kwenye viwanja viwili tofauti.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa na CECAFA  asubuhi hii, Victoria University kutoka nchini Uganda atakabiliana na Malakia FC kutoka Sudan Kusini katika uwanja wa Al-Merreikh mjini Khartoum majira ya saa 11:30 jioni.
Baadaye katika uwanja huo huo, wenyeji, Al-Merreik wataoneshana kazi na timu ya Polisi kutoka visiwani Zanzibar majira ya saa 2:00 usiku.
Mbali na mechi hizo za Khartoum, mechi nyingine itapigwa mjini Shandi, ambapo wenyeji Al-Shandi watavaana na wageni, Dkhill FC kutoka nchini  Djibouti.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com

0 comments: