Friday 23 May 2014

HUU NDIO UKWELI KUHUSU MADINI YALIYONDULIKA LOLIONDO NI DHAHABU

Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro asema hakuna udhibitisho kama kweli madini yaliyogundulika Loliondo ni dhahabu

dhahabu+jiwe 
Mahmoud Ahmad Arusha
MKUU wa Wilaya ya Ngorongoro, Elias  Wawalali amesema kuwa  bado haijathibitishwa kama madini yanayodaiwa kugundulika Kijiji cha Mgongo
ni dhahabu au la na kusisitiza kuwa idadi ya watu wanaofika  wilayani hapo ni ndogo  haifanani na msimu ule wa kikombe cha Babu wa Loliondo
Wawalali alilazimika kutoa ufafanuzi huo jana Jijini hapa wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari
waliotaka kujua je ni kweli madini hayo yanapatikana juu juu kama habari zinavyoandikwa.

Alisema ni kweli madini yamegundulika lakini bado hayajathibitishwa kama madini hayo ni dhahabu kweli au ni madini ya aina nyingine na
muda wowote kuanzia sasa wataalam wa madini Kanda ya Kaskazini watatoa taarifa juu ya aina ya madini waliyoyagundua kwani timu ya wataalam
imeshafika eneo hilo kwaajili ya kuchunguza na kutoa elimu ya uchimbaji wa madini hayo.

Alisema awali wakati taarifa hizo zimetoka kuwa madini yanapatikana nje nje karibu na mto Mgongo alifika eneo hilo  akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama  ili kujua kama ni kweli au la lakini waligundua kuwa madini hayo si kweli yapo juu juu kama inavyodaiwa bali waliwakuta wachimbaji wadogo wanaoshi maeneo hayo wakiwa wanachimba madini hayo pembezoni mwa mto.
Alisema idadi ya watu si kubwa kama inavyodaiwa bali watu waliopo ni 400 hadi 600  huku asilimia 80  ya idadi ya watu hao ni wakazi wa Kijiji cha Mgongo, asilimia 10 ni wale wanaotoka ndani ya Wilaya ya Samunge  huku asilimia 5 ni wale wanaotoka nje ya wilaya hiyo na asilimia 5 ni wale wanaotoka ndani ya Wilaya ya Ngorongoro.
Alisema bado hawajapata uhakika ni dhahabu kweli au la  bali wanachosubiriwa na majibu ya uhakika kutoka kwa wataalam kama kweli ni dhahabu au la  lakini hivi sasa wamejipanga kuhakikisha kuwa huduma muhimu za  ulinzi na usalama zinakuwepo ikiwemo maji ,huduma za vyoo na nk.
Alisema ingawa maji katika eneo hilo ni shida lakini watahakikisha maji yanapatikana na huduma nyingine maana watu wakishasikia masuala kama ya dhahabu wanaweza kuja kwa wingi na ikawa kama yale ya Samunge hivyo wanajipanga kuhakikisha huduma muhimu zitapatikana endapo watadhibitishiwa kama kweli kunadhahabu imegunduliwa.
“Napigiwa simu hadi usiku wa manane juu ya suala hili la madini ya dhahabu ukweli bado hayajathibitishwa bali ni hisia tu mpaka wataalam
wadhibitishe hilo ila watu wanaendelea kuchimba pembezoni mwa  mto na juu ya mlima uliopo eneo la kijiji cha Mgongo”.

Wawalia aliongeza kuwa  kugundulika kwa madini hayo kusifananishwe na Kikombe cha Babu na kusisitiza kuwa ni kweli madini hayo yapo lakini
bado hayajathibitishwa rasmi kama ni dhahabu au la na kutoa rai kwa watu wanaopenda kutoa taarifa hata kama ni za kweli wawasiliane na mamlaka husika ili kutoa taarifa za uhakika badala ya kutoa taarifa wanazozijua wao.

0 comments: