Friday 23 May 2014

DAVID LUIZ KUTUA PSG KWA DAU LA REKODI DUNIA NZIMA HAIJAWAHI KUTOKEA KWA BEKI

BEKI David Luiz yuko njiani kujiunga na Paris St Germain ndani ya saa 48 zijazo katika uhamisho ambao utaigharimu klabu hiyo kibopa Ufaransa kiasi cha Pauni Milioni 50.

Klabu hizo mbili zimekwishaafikiana juu ya vipengele muhimu, lakini uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 wa Chelsea utakuwa usajili wa bei mbaya zaidi kwa beki duniani ukipiku rekodi za usajili wa mabeki wengie waliosajiliwa awali PSG, Marquinhos na Thiago Silva.
Mara baada ya kukamilishiana na kila kitu na klabu ya Stamford Bridge, PSG itaomba ruhusa kwa kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari kwenda kwenye kambi yao ya maandalizi ya Kombe la Dunia kumfanyia vipimo vya afya kabla ya kumsainisha.
Kwaheri: David Luiz akiwapungia mono mashabiki katika tukio la Kombe la Dunia mjini Sao Paulo, Brazil Jumanne.

0 comments: