Friday 23 May 2014

RONALNADO NA BALE : KESHO LISBON PATACHIMBIKA KWENYE FAINALI YA CL

 
Ronaldo na Bale kuchuana dhidi ya Atletico Madrid
Mchezaji bora duniani mwaka huu Cristiano Ronaldo na mshambulizi aliyegharimu kitita kikubwa zaidi duniani Gareth Bale watakuwepo katika timu ya Real Madrid itakayochuana na Atletico Madrid katika fainali ya kuwania kombe la mabingwa barani Uropa jumamosi hii.
Ronaldo, 29, alikuwa amekosa kucheza mechi mbili akiuguza jereha sawa na mshambulizi Gareth Bale, 24, ambaye hakushiriki katika mazoezi siku ya jumanne.
Wawili hao kwa ushirikiano wamiefungia Real Madrid mabao 68 msimu huu.
Kocha Carlo Ancelotti, ambaye anapania kuwa mkufunzi wa pili katika historia ya mchuano huu kuwahi kushinda taji la ubingwa barani Ulaya mara tatu amethibitisha kuwa nyota hao wawili wakali kwa mashambuli watakuwepo
Ronaldo atacheza dhidi ya Atletico Madrid
Lisbon huku akiongezea kuwa anasubiri ithibati ya muuguzi wa timu kuhakiki kuwepo kwa mlinzi Pepe na mshambulizi Karim Benzema.
Benzema alijeruhiwa Real ilipoibana Espanyol 3-1 huku Pepe akisalia kwenye bench kwa zaidi ya majuma mawili sasa.
Real Madrid inapania kutawazwa mabingwa wa Uropa iwapo watawalaza washindi wapya wa ligi kuu ya Uhispania Atletico Madrid mbali na kusitisha ukame wa miaka 12 wa kombe hilo lenye umaarufu barani Uropa.
Aidha fainali hii baina ya mahasimu hao wa jadi wanaootokea mji wa Madrid itakuwa ya kwanza katika historia ya kombe hili kujumuisha wapinzani wa ligi ya nyumbani.
Atletico wamechuana dhidi ya Real Madrid mara nne msimu huu ,Real ikishinda mechi za kuwania kombe la Spanish kwa mabao 5-0 huku Atletico ikiibuka na ushindi katika mechi za ligi ya Uhispania .
Atletico kwa upande wake inasubiri kujua hali ya siha ya mshambulizi wake Diego Costa ambaye alijeruhiwa mapema katika mechi ya kuamua mshindi wa la Liga dhidi ya Barcelona mwishoni mwa juma.

0 comments: