Monday 26 May 2014

Wananchi Arusha washinda kesi dhidi ya Halmashauri ya wilaya

9.
Mahmoud Ahmad Arusha
Wananchi waishio kata ya Elkiding’a wilaya ya Arusha wameshinda kesi kwenye mahakama kuu ya mkoa wa Arusha dhidi ya Halmashauri ya wilaya hiyo leo(jana) jijini hapa mbele ya jaji mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Arusha.
 
Kesi hiyo no.18 ya mwaka 2013 waliokuwa wakiilalamikia halmashauri ya Arusha kuvunja nyumba zao pamoja na kung’oa miti iliyokuwa pembezoni mwa barabara ya Mianzini hadi kijiji cha Timbolo ilizua furaha na machozi ya furaha kwa wananchi hao mahakamani hapo.
 
Akisoma hukumu hiyo Jaji mfawidhi Bi Fatuma Masengi aliitaka halmashauri hiyo kuleta watathmini ndani ya miezi mitatu kupitia uharibufu waliofanya wa kuvunja nyumba hizo za wananchi waliokuwa pembezoni mwa barabara hiyo.
 
Wakiwa na nyuso za furaha wananchi hao zaidi ya 43 mmoja wa viongozi ambao walikuwa wakiifuatilia kesi hiyo Fanuel Taitus alisema kuwa haki imetendeka na imeonyesha kuwa mahakama hiyo chini ya majaji wanawake inaendeshwa kwa mujibu wa sheria za nchi na wanaimani nao.
 
Taitus Akatanabaisha kuwa halmashauri hiyo ya Arusha zamani  Arumeru ilishindwa kukaa nao kujua na kutathmini mali zao ili waweze kufidiwa na kuwa walitumia mabavu kwani wao pia ni wadau wamaendeleo hivyo hawakatai maendeleo ila walitaka haki itendeke pale maendeleo yanaposogea kwenye vijiji vyao.
 
“Sisi sasa tunangoja utekelezaji wa hukumu ndani ya miezi mitatu waliopewa halmshauri kuleta watathmini kuja kukagua ilituweze kupata haki yetu kwani pia maendeleo ni yetu sote ila tumekosa makazi na sehemu za kwenda kuishi”alisema Taitus.
 
Juhudi za kumpata mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Arusha Phidelis  Lumato zilishindikana kwani alikuwa nje ya ofisi na simu yake ilikuwa ikiita bila majibu na juhudi zinaendelea ilikupata ufafanuzi wa hukumu ya mahakama.

0 comments: