Friday 23 May 2014

MWENYEKITI CCM WILAYA NJOMBE AFARIKI GHAFLA


late_65549.jpg
Aliekuwa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe, Adam Ismail Msigwa (pichani) ambaye alijukana kwa jina maarufu kama 'Shilingi ni Vita' amefariki jana usiku wa kuamkia leo nyumbani katika Mitaa wa Kwivaha Njombe mjini na mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho kijijini kwake Lusitu.
Marehemu Adam Msigwa ambaye ni baba mlezi wa mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Iringa, Jesca Msavatavangu ambaye ni mjombe wake spika wa bunge Anna Makinda amefarika dunia jana usiku wa kuamkia leo baada ya kufariki ghafla kwa ugonjwa wa shinikizo la damu (BP) pamoja na matatizo ya moyo.
msiba_e3922.jpg
Mwenyekiti wa Wilaya ya Njombe mjini, Adam Msigwa (mwenye kofia) enzi za uhai wake akiwa na Mkuu wa Wilaya Njombe Sarah Dumba wakati wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka jana.
mramba_c071f.jpg
mkuu_16922.jpg
mkapa_f85d4.jpg
 (NA FRIDAY SIMBAYA, NJOMBE)

0 comments: