Tuesday, 5 November 2013

UEFA CHAMPIONS LIGI TIMU 4 ZA SHUKA UWANJANI LEO USIKU KUSAKA USHINDI

NI MABINGWA  BAYERN, REAL, PSG & ATLETICO, 

ZOTE ZIMESHINDA 3 ZA MWANZO!

PIA WAMO BARCA, MAN CITY WANAOWEZA KUFUZU WIKI HII!
UCL_2013_LOGO 
MABINGWA Watetezi Bayern Munich, Mabingwa wa Ulaya mara 9 Real Madrid, Paris St Germain na Atletico Madrid zote zimeshinda Mechi zao zote 3 za Makundi yao ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, na Wiki hii wakishinda Mechi zao za 4 basi watatinga Raundi ijayo ya Mtoano wakiwa na Mechi mbili mkononi.

Mbali ya Timu hizo 4, Manchester City, ambao wameshinda Mechi mbili za Kundi D na kufungwa moja, pia wanaweza kusonga mbeli ikiwa wataifunga CSKA Moscow Jumanne Usiku na wakati huo huo Mabingwa Bayern kuifunga Viktoria Plzen.

Barcelona, ambao wamepoteza Pointi 2 baada kwenda Sare ya Bao 1-1 na AC Milan kwenye Kundi H, wanaweza kufuzu ikiwa wataifunga AC Milan Uwanjani Nou Camp hapo Jumatano na matokeo mengine kwenye Kundi kuwa mazuri kwao.
Nao Mabingwa wa England, Manchester United, ambao Jumanne Usiku wako Ugenini huko Spain, watapiga hatua kubwa kufuzu ikiwa wataifunga Real Sociedad Timu ambayo kwenye Kundi A imefungwa Mechi zao zote 3.

Lakini, kwenye Makundi ambayo wamo Arsenal na Chelsea, mambo bado magumu na labda mwelekeo utaonekana baada Mechi za 4 kumalizika.

Arsenal wako Kundi F ambalo Vinara ni Borussia Dortmund wakifuatia Arsenal kisha Napoli lakini Timu zote hizi zina Pointi 6 kila mmoja na Marseille yuko mkiani akiwa hana hata Pointi.
Chelsea wako Kundi E wakiongoza na Pointi 6 sawa na Schlake na Nafasi ya Tatu ni FC Basel wenye Pointi 4 na mkiani ni Steau Bucharest wenye Pointi moja tu.

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

RATIBA:
MECHI ZA 4 ZA MAKUNDI  
Jumanne 5 Nov 2013

[Mechi zote Saa 4 Dakika 45 Usiku]
FC Shakhtar Donetsk v Bayer 04 Leverkusen
Real Sociedad de Fútbol v Manchester United FC
Juventus v Real Madrid CF
FC København v Galatasaray A.Ş.
Paris Saint-Germain v RSC Anderlecht
Olympiacos FC v SL Benfica
Manchester City FC v PFC CSKA Moskva
FC Viktoria Plzeň v FC Bayern München

Jumatano 6 Nov 2013
[Mechi zote Saa 4 Dakika 45 Usiku isipokuwa inapotajwa]

FC Basel 1893 v FC Steaua Bucureşti
Chelsea FC v FC Schalke 04
Borussia Dortmund v Arsenal FC
SSC Napoli v Olympique de Marseille
Football Club Zenit v FC Porto [Saa 2 Usiku]
Club Atlético de Madrid v FK Austria Wien
AFC Ajax v Celtic FC
FC Barcelona v AC Milan

XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

Mabingwa Bayern Munich watakuwa Ugenini kurudiana na Klabu ya Czech Republic Viktoria Plzen, waliyoinyuka 5-0 Wiki mbili zilizopita huko Munich.

Paris St Germain wako Nyumbani kurudiana na Anderlecht waliyoitwanga  5-0 huko Brussels.
Real Madrid, ambao waliifunga Juventus 2-1 Wiki mbili zilizopita, wanasafiri kwenda Turin kurudiana nao.
Baada ya kuichapa Ugenini 3-0, Atletico Madrid wako kwao kucheza tena na Austria Vienna.
Manchester City, ambao wako Nafasi ya Pili kwenye Kundi D nyuma ya Bayern Munich, watafuzu kuingia Raundi ya Mtoano ikiwa wataifunga CSKA.

Wakishinda Man City , huku Bayern wakiichapa Viktoria Plzen, watakuwa na Pointi 9 baada ya Mechi 4 na hata kama watafungwa Mechi zilizosalia na CSKA kuzifikia Pointi hizo 9 City watafuzu kwa vile Rekodi ya uso kwa uso kati yao na CSKA ni nzuri.

UEFA CHAMPIONZ LIGI

MSIMAMO:
KUNDI A

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Manchester United 3 2 1 0 6 3 3 7
2 Bayer 04 Leverkusen 3 2 0 1 8 5 3 4
3 FC Shakhtar Donetsk 3 1 1 1 3 5 -2 4
4 Real Sociedad 3 0 0 3 1 5 -4 0
KUNDI B

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Real Madrid CF 3 3 0 0 12 2 9 9
2 Galatasaray Spor Kulübü 3 1 1 1 6 9 0 4
3 Juventus 3 0 2 1 4 5 -4 2
4 FC Copenhagen 3 0 1 2 2 8 -5 1
KUNDI C

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Paris Saint-Germain 3 3 0 0 12 1 6 9
2 Olympiacos CFP 3 1 1 1 5 5 0 4
3 Benfica 3 1 1 1 3 4 10 4
4 RSC Anderlecht 3 0 0 3 0 10 -5 0
KUNDI D

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Bayern Munich 3 3 0 0 11 1 10 9
2 Manchester City 3 2 0 1 6 4 2 6
3 CSKA Moskva 3 1 0 2 4 7 -3 3
4 FC Viktoria Plzen 3 0 0 3 2 11 -9 0
KUNDI E

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Chelsea FC 3 2 0 1 8 2 4 6
2 Schalke 3 2 0 1 4 3 3 6
3 FC Basel 1893 3 1 1 1 3 3 0 4
4 FC Steaua Bucuresti 3 0 1 2 1 8 -7 1
KUNDI F

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 BV Borussia Dortmund 3 2 0 1 6 3 3 6
2 Arsenal 3 2 0 1 5 3 2 6
3 Napoli 3 2 0 1 4 4 0 6
4 Olympique de Marseille 3 0 0 3 2 7 -5 0
KUNDI G

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Atletico de Madrid 3 3 0 0 8 2 6 9
2 Zenit St. Petersburg 3 1 1 1 2 3 -1 4
3 FC Porto 3 1 0 2 2 3 -1 3
4 FK Austria Wien 3 0 1 2 0 4 -4 1
KUNDI H

















NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 FC Barcelona 3 2 1 0 6 1 5 7
2 AC Milan 3 1 2 0 4 2 2 5
3 Celtic 3 1 0 2 2 4 -2 3
4 Ajax Amsterdam 3 0 1 2 2 7 -5 1

0 comments: