TANZANITE KWENDA MAPUTO JUMATANO!
TFF YATAKA ORODHA YA WALIOSAMEHEWA
PATA TAARIFA KAMILI/MSIMAMO WA LIGI:
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
Release No. 190
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Novemba 5, 2013
ASHANTI UTD, SIMBA UWANJANI VPL
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza
wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) zinaanza kesho (Novemba 6 mwaka huu) ambapo
Ashanti United itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo
itakayochezwa kuanzia saa 10 kamili chini ya mwamuzi Andrew Shamba
kutoka Pwani ni sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000. Waamuzi
wasaidizi ni Abdallah Mkomwa na Rashid Abdallah wote kutoka Pwani wakati
mezani atakuwa Hamisi Chang’walu.
Mechi nyingine za kesho ni JKT Ruvu
Stars na Coastal Union (Uwanja wa Chamazi), Kagera Sugar na Mgambo
Shooting (Uwanja wa Kaitaba, Bukoba) na Ruvu Shooting na Mtibwa Sugar
(Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Keshokutwa (Novemba 7 mwaka huu) raundi
ya 13 kumaliza mzunguko wa kwanza itakamilika kwa mechi kati ya Yanga na
Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa kwa viingilio vya sh. 5,000, sh.
8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000.
Azam itakuwa mwenyeji wa Mbeya City
kwenye Uwanja wa Chamazi wakati Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora
utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Rhino Rangers na Tanzania Prisons
kutoka Mbeya.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na
Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.
TFF YATAKA ORODHA YA WALIOSAMEHEWA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limetuma waraka kwa vyama vya mpira wa miguu vya wilaya, mikoa na
vyama shiriki kuvitaka kuwasilisha orodha ya wote waliofaidika na
msamaha wa Oktoba 28 mwaka huu.
Oktoba 28 mwaka huu wakati akizungumza
katika Mkutano Mkuu baada ya uchaguzi, Rais mpya wa TFF, Jamal Malinzi
alitoa msamaha kwa wote waliofungiwa kwa sababu mbalimbali.
Hata hivyo, msamaha huo hauwahusu
waliofungiwa kutokana na makosa ya rushwa au kupanga matokeo. Vilevile
haugusi adhabu zilizotolewa ndani ya klabu.
Vyama vya mikoa vinatakiwa kuhakikisha
waraka huo unafika kwa wanachama wao (vyama vya mpira wa miguu vya
wilaya). TFF inataka orodha ya wote waliofaidika na msamaha huo kwa
ajili ya kumbukumbu zake (records).
TANZANITE KWENDA MAPUTO KESHO
Kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake
chini ya miaka 20 (Tanzanite) kinaagwa kesho (Novemba 6 mwaka huu) saa
chache kabla ya kuanza safari ya kwenda Maputo, Msumbiji.
Hafla fupi ya kuikabidhi bendera
Tanzanite itafanyika kesho saa 5 asubuhi kwenye ofisi za TFF wakati
kikosi hicho kinatarajiwa kupaa saa 11 jioni kwa ndege ya LAM na
kuwasili Maputo saa 3.45 usiku.
Msafara wa Tanzanite ambayo ilishinda
mechi ya kwanza mabao 10-0 karibu wiki mbili zilizopita jijini Dar es
Salaam utaongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Kidao Wilfred.
Mechi hiyo ya marudiano itachezwa
Novemba 9 mwaka huu Uwanja wa Taifa wa Zimpeto, na timu itarejea
nyumbani Novemba 10 mwaka huu saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
LIGI KUU VODACOM
MSIMAMO:
NO
|
TEAMS
|
P
|
W
|
D
|
L
|
GF
|
GA
|
GD
|
PTS
|
1
|
Azam FC |
12
|
7
|
5
|
0
|
20
|
7
|
13
|
26
|
2
|
Mbeya City |
12
|
7
|
5
|
0
|
17
|
8
|
9
|
26
|
3
|
Young Africans |
12
|
7
|
4
|
1
|
28
|
11
|
17
|
25
|
4
|
Simba SC |
12
|
5
|
6
|
1
|
22
|
11
|
11
|
21
|
5
|
Mtibwa Sugar |
12
|
5
|
4
|
3
|
17
|
15
|
2
|
19
|
6
|
Kagera Sugar |
12
|
4
|
5
|
3
|
13
|
10
|
3
|
17
|
7
|
Coastal Union |
12
|
3
|
7
|
2
|
10
|
6
|
4
|
16
|
8
|
Ruvu Shootings |
12
|
4
|
4
|
4
|
13
|
13
|
0
|
16
|
9
|
JKT Ruvu |
12
|
4
|
0
|
8
|
9
|
16
|
-7
|
12
|
10
|
Rhino Rangers |
12
|
2
|
4
|
6
|
9
|
16
|
-7
|
10
|
11
|
JKT Oljoro |
12
|
2
|
4
|
6
|
9
|
16
|
-7
|
10
|
12
|
Ashanti United |
12
|
2
|
4
|
6
|
10
|
20
|
-10
|
10
|
13
|
Tanzania Prisons |
12
|
1
|
5
|
6
|
6
|
16
|
-10
|
8
|
14
|
Mgambo JKT |
12
|
1
|
3
|
8
|
3
|
21
|
-18
|
6
|
|
TOTAL
|
84
|
27
|
30
|
27
|
186
|
186
|
0
|
222
|
0 comments:
Post a Comment