Kocha Rogasian Kaijage
Timu
ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza
raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya
mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao
5-1.
Mabao
ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto
jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu
(hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia
Minja.
Msafara
wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo Jumapili (Novemba 10
mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
0 comments:
Post a Comment