KAMBI
ya Holland imethibitisha kuwa Straika wa Manchester United Robin van
Persie ana maumivu na hivyo kuzikosa Mechi za Nchi hiyo na huko Denmark,
Kocha Mkuu amemtaka Straika wa Arsenal Nicklas Bendtner aihame Klabu
yake.
SOMA HAPA UPATE UHONDO ZAIDI:
ROBIN VAN PERSIE AZIKOSA MECHI ZA HOLLAND
KAMBI ya Holland imethibitisha kuwa
Straika wa Manchester United Robin van Persie ana maumivu ya Kidole cha
Mguuni na pia kwenye Nyonga na hivyo hatakuwa fiti kucheza Mechi za
Kirafiki za Nchi hiyo baadae Wiki hii dhidi ya Japan na Colombia.
Jumapili iliyopita, Van Persie alicheza
Dakika 85 za Mechi ya Klabu yake walipoifunga Arsenal Bao 1-0 huku yeye
ndie Mfungaji wa Bao hilo.
Ikiwa maumivu ya Staa huyo yataendelea
anaweza kuikosa Mechi ijayo ya Man United ya Ligi Kuu England Ugenini na
Cardiff City hapo Jumapili Novemba 24.
Baada ya Mechi hiyo zitafuata Mechi ya
UEFA CHAMPIONZ LIGI na Bayer Leverkusen, kisha Mechi za Ligi Kuu England
dhidi ya Tottenham na Everton.
BENDTNER ATAKIWA KUHAMA ARSENAL
Straika wa Denmark Nicklas Bendtner ameambiwa na Kocha wa Nchi hiyo, Morten Olsen, aihame Arsenal kwenye Dirisha la Uhamisho la Januari.
Bendtner, mwenye Miaka 25, alitarajiwa
kuihama Arsenal kabla Msimu huu kuanza baada ya kuwa kwa Mkopo huko
Sunderland na Juventus katika Misimu miwili iliyopita lakini Arsenal
ikamtaka abaki.
Bendtner, ambae alijiunga na Arsenal
toka akiwa na Miaka 16 akitokea FC Copenhagen, Msimu huu amecheza Mechi 7
za Arsenal lakini hajafunga na Bao zake pekee Msimu huu ni zile
alizoifungia Denmark Bao mbili walipotoka Sare ya 2-2 na Italy kwenye
Mechi ya Kombe la Dunia.
Na Kocha Olsen, ambae anahisi Bendtner
anadumazwa huko Arsenal, amesema: “Bendtner alitufungia Goli mbili safi
lakini kwenye Mechi ile alionyesha udhaifu na hilo linakuja tu kwa
sababu ya kukosa kucheza Mechi mfululizo. Na kwa sababu hiyo tu ni
lazima atafute Klabu nyingine. Wanasoka wanataka kucheza Soka!”
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 23 Novemba
1545 Everton v Liverpool
1800 Arsenal v Southampton
1800 Fulham v Swansea City
1800 Hull City v Crystal Palace
1800 Newcastle United v Norwich City
1800 Stoke City v Sunderland
2030 West Ham United v Chelsea
Jumapili 24 Novemba
1630 Manchester City v Tottenham Hotspur
1900 Cardiff City v Manchester United
Jumatatu 25 Novemba
2300 West Bromwich Albion v Aston Villa
Kwahisani ya soka inbongoblog
Tuesday, 12 November 2013 17:05
0 comments:
Post a Comment