Nchini
Uganda, shabiki mmoja sugu wa timu ya soka ya Arsenal ya nchini
Uingereza amepoteza nyumba yake baada ya kuwekeana dau na shabiki
mwenziye wa timu pinzani ya Manchester United katika mechi iliyochezwa
juzi Jumapili.
Kabla ya mechi hiyo kuchezwa uwanjani Old Trafford hiyo juzi, Henry Dhabasani alikubali kutoa nyumba yake ya vyumba

viwili kwa Rashid Yiga iwapo Arsenal ingecharazwa na ManU katika mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza. Yeye Yiga alikubali kutoa gari lake aina ya Toyota Premio
pamoja na mkewe iwapo ManU ingetandikwa katika mechi hiyo.
“Wawili hao waliandika mkataba huo machoni mwa mashabiki na viongozi wa kijiji,” gazeti la Observer limeripoti.
Inaripotiwa kuwa, baada ya ManU kuilabua Arsenal 1:0, ndugu Dhabasani, baba wa watoto watano na mume wa wake watatu, alizirai.
Siku iliyofuata baada ya mechi, mashabiki wa Man United walifika kwa Dhabasani Jumatatu na kumfurusha pamoja na jamii yake na sasa, amebaki akitafuta nyumba nyingine.

0 comments:
Post a Comment