TAKWIMU za taifa kuhusu demografia na afya ya jamii zimeonyesha
upungufu wa Vitamin A unaathiri asilimia 33 ya watoto walio chini ya
miaka mitano na asilimia 37 wanawake walio na umri wa kuzaa.
Takwimu hizo zilitolewa jijini Dar es Salaam jana na Elifatio Towo
kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, aliyeeleza kwamba njia ya
kupunguza tatizo hilo ni kutumia teknolojia ya kuongeza vitamin na
madini katika vyakula vikuu ambavyo ni unga wa ngano, sukari, mafuta ya
kupikia na unga wa mahindi.
Towo alisema ili teknolijia hiyo ipate matokeo mazuri ni vema viwango
sahihi vya uongezaji wa vitamin na madini katika chakula vikafanyika
kwa uangalifu zaidi ikiwemo udhibiti, usimamizi na tathmini ya mpango
wa uongezaji virutubisho kwa ngazi zote.
Alizitaja changamoto wanazokabiliana nazo ni pamoja na upelekaji
elimu sahihi juu ya mpango wa kuongeza virutubisho vya chakula kwenye
jamii, ikihusisha na mambo mengine ikiwamo kupunguza uzazi wa mpango.
Changamoto nyingine ni kutokuwa na mfumo wa usambazaji wa vyakula,
hali inayosababisha walengwa kuvipata kwa usumbufu na utambuzi wa
vyakula vilivyoongezwa virutubishio bado haujaeleweka kwa jamii.
na Happiness Mnale TANZANIA DAIMA GAZETI
0 comments:
Post a Comment