Monday, 3 March 2014

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA KUSIMAMIA MARADI WA KUPASHANA HABARI

hd_2_7c4ef.png
Mwakilishi wa Tanzana katika mkutano huo Ndg. Phares Magesa ambaye ni Mkurugenzi wa ICT- TPA akiwa mkutanoni katika ukumbi wa Umoja wa Ulaya, Brussels.
Tanzania yashiriki mkutano wa 3 wa kamati ya kusimamia mradi wa kupashana habari ili kupambana na uhalifu baharini, 3rd Maritime Security & Safety Information Sharing for Capacity building (MARSIC ) unaofanyika kwa kuratibiwa na Umoja wa Ulaya , Brussels, Ubelgji 3-4 Machi, 2014.
Tanzania ni moja ya nchi zenye vituo hivyo vya kupashana habari (Informations Sharing Centres) kilichopo katika Mnara wa kupngoza Meli cha Feri (Control Tower) kinaendeshwa na TPA kwa kushirikiana na Sumatra na idara nyingine za ulinzi na Usalama za Serikali kiutekelezaji.
hd_3_59c79.jpg
hd_1_2441c.png
baadhi ya wajumbe kutoka nchi mbali mbali wakiwa mkutanoni.
Vituo vingine vya mradi huo viko Djibouti, Mombasa - Kenya na Sanaa -Yemen katika ukanda wa bahari ya Hindi.
Picha, maelezo na Phares Magesa

Related Posts:

0 comments: