Bastola iliyotumika katika shambulizi hilo. Picha na Sammy Kimatu wa Daily Nation.
Na Fadhy Mtanga
AFISA wa
Jeshi la Polisi nchini Kenya amemjeruhi vibaya mkewe kabla hajajiua.
Tukio hilo lilijiri majira ya saa saba unusu usiku ndani ya makazi yao
huko South B, Nairobi.
Gazeti la
Daily Nation la nchini humo limeripoti kuwa, kabla ya tukio hilo askari
huyo mwenye cheo cha Sajini Mwandamizi katika ofisi za Westlands,
alirejea nyumbani usiku wa manane na kuanza ugomvi na mkewe. Taarifa
zinaeleza kuwa ugomvi huo ulihusu kodi ya pango walilokuwa wakiishi.
Sajini
Mwandamizi huyo alimdai mkewe kiasi cha shilingi za Kenya 16,000
alizokuwa amempa kabla kwa ajili ya kulipia pango kwa mwezi huu Machi.
Hata hivyo, mkewe hakuweza kutoa kiasi hicho cha pesa wala kuwa na
maelezo yaliyotosheleza.
Kwa
mujibu wa jirani yao, Peter Thuita, kulisikika yowe zilizofuatiwa na
mlio wa risasi majira ya saa tisa usiku kutoka nyumbani kwa afisa huyo
wa polisi.
Mkuu wa
Upelelezi eneo la Makadara, Zach Nanguli amesema kuwa afisa wake huyo
alirejea nyumbani mapema isivyo kawaida lakini akiwa tayari ameutwika
kiasi cha kutosha. Kisha, akamtwanga mkewe risasi tano ikiwa ni
shingoni, mguuni, mkononi, begani na tumboni kabla mwanamke huyo
hajafanikiwa kujinusuru kwa kukimbilia nje ya nyumba hiyo. Baada ya
hapo, afisa huyo akajitwanga risasi kichwani na kufariki papo hapo.
Mwanamke
huyo anayefahamika kwa jinala Janet Atieno, alikimbizwa hospitalini
Mariakani akiwa mahututi. Mwanamke huyo pia ni afisa wa polisi akiwa na
cheo cha Konstebo akihusika zaidi na ulinzi wa majengo ya serikali
katika eneo la Uhuru.
Silaha ya
Sajini Mwandamizi, bastola ikiwa na risasi saba ilipatikana katika eneo
la tukio. Afisa Upelelezi amesema pia walikuta maganda nane ya risasi
zilizotumika.
Afisa
huyo aliyejiua aliandika katika ukurasa wake wa FAcebook muda mfupi
kabla ya zahma hiyo. Aliandika, "Lazima nifanye jambo la kijinga. Liwe
liwalo. Nimechoka
0 comments:
Post a Comment