Friday, 7 March 2014

CAF CHAMPIONZ LIGI KUANZA LEO, AL AHLY v YANGA JUMAPILI,

YANGA_v_ALAHLYPATASHIKA ya Mechi za Marudiano za Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI zinaanza Leo hii huko Angola ambako Kabuscorp ya Nchi hiyo itarudiana na Al Zamalek ya Egypt huku ikiwa nyuma kwa Bao 1-0.
Mechi nyingine za Marudiano zitachezwa Jumamosi na Jumapili huku Mabingwa Watetezi Al Ahly wakiwa huko Harras El-Hedoud Stadium Mjini Alexandria hapo Jumapili kurudiana na Yanga huku wakiwa nyuma kwa Bao 1-0.
Katika Mechi ya Kwanza, Al Ahly walifungwa Bao 1-0 Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Wiki iliyopita kwa Bao lilofungwa na Nadir Haroub "Cannavaro".
Kwenye Raundi ya Pili, Mshindi wa Mechi hii ya Al Ahly na Yanga atapambana na Mshindi kati ya Al Ahli - Benghazi ya Libya v Berekum Chelsea ya Ghana ambazo zilitoka 1-1 katika Mechi ya Kwanza.
PATA RATIBA/MATOKEO MECHI ZA KWANZA:CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Kwanza
Marudiano
[Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Ijumaa Machi 7
Kabuscorp – Angola v Al Zamalek – Egypt [0-1]
Jumamosi Machi 8
Kampala City Council FC – Uganda v Nkana FC – Zambia [2-2]
Coton Sport FC – Cameroon v Flambeau de l’Est – Burundi [0-0]
ASFA-Yennenga - Burkina Faso v Entente Sportive de Sétif - Algeria [0-5]
Liga Muculmana de Maputo – Mozambique v Kaizer Chiefs - South Africa [0-4]
Primeiro de Agosto – Angola v AC Leopards de Dolisie – Congo [1-4]
AS Bamako – Mali v Enyimba International FC – Nigeria [2-1]
Raja Club Athletic – Morocco v Horoya Athlétique Club – Guinea [0-1]
Jumapili Machi 9
Al Ahly – Egypt v Young Africans – Tanzania [0-1]
Al Ahli - Benghazi – Libya v Berekum Chelsea - Ghana [1-1]
TP Mazembe - Congo, DR v Les Astres de Douala – Cameroon [1-1]
AS Vita Club - Congo, DR v Dynamos – Zimbabwe [0-0]
Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v Gor Mahia – Kenya [3-2]
Sewe Sport - Ivory Coast v Barrack Y.C.II – Liberia [3-3]
Al-Hilal – Sudan v Stade Malien de Bamako – Mali [0-0]

Related Posts:

0 comments: