Saturday 17 May 2014

LUIZ SUAREZ ATHIBISHA KWA KUSEMA HAONDOKI LIVERPOOL

 
MSHAMBULIAJI Luis Suarez amesema anapenda maisha ndani ya Liverpool na hafikirii kuondoka Anfield.
Nyota huyo wa Uruguay amemaliza msimu vizuri akiwa na Wekundu hap kwa kufunga mabao 31 na kutwaa tuzo za Mwanasoka Bora wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa (PFA) na ya Waandishi wa Habari za Soka.
Mafanikio hayo yanakuja baada ya kupitia msimu mgumu uliopita akifungiwa kwa kumng'ata beki wa Chelsea, Branislav Ivanovic - akilazimisha kupita.
Siondoki: Mshambuliaji Luis Suarez amesema hana mpango wa kuondoka Liverpool licha ya kutakiwa na vigogo wa La Liga, Real Madrid na Barcelona

Sasa wakati tetesi za usajili zimeanza tena, Suarez, ambaye mapema wiki hii alikanusha kuwa na nia ya kuhamia klabu nyingine kubwa Ulaya, ameamua kuuheshimu mkataba aliosaini Desemba mwaka jana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye ameripotiwa kutakiwa na Real Madrid, ameiambia Sky Sports kwamba: "Nilisaini mkataba kwa sababu napapenda haps na nina furaha dana hapa. Ikiwa haunt furaha hapa huwezi kusaini mkataba wowote,".
"Liverpool kwangu ni moja ya timu bora duniani, kwa sababu hakuna mtu haps katika chumba cha kubadilishia nguo anafikiri mimi no bora zaidi ya wengine na watu hapa ndani ya Melwood wanafanya kazi vizuri,"alisema.

0 comments: