Saturday 17 May 2014

KATIBU WA UWT MKOA WA MBEYA APOKELEWA KWA MIKONO MIWILI KATKA WILAYA YA MBEYA MJINI




Umoja wa wanawake Tanzania (uwt) wilaya  mbeya mjini  kimefanya kikakao cha baraza la uwt( w)  kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa ccm kata ya sisimba  mkoani mbeya  ,kikao hicho kilihudhuri  na wenye viti wa uwt kata na wajumbe wa wiliya wa umoja huo
Malengo ya kikao hicho ni kumkalibisha katibu mpya wa uwt mkoa,kuimalisha uhai wa umaja huo,kuahamashana kwa shughuli mabalimabali za umoja huo na kuanzisha miradi ya uwt wilaya
  Uwt wilaya ya mbeya mnjini wamemmpokea kwa mikono miwili katibu wao mpya  wa umoja huo bibi MARIMA YUSUFU  katika mkoa mbeya, hii nibaada ya mabadiriko ya umoja huo ulio fanyika  hapa nchini  bi mariam amechukua na fasi  TABU RUGWESYA alikuawa katibu wa UWT  mkoa wa mbeya
Katika kikao hicho bibi mariam  meowamba wanawake wote, na wanyeviti wa kata kuitisha vikao kulingana na katiba ya chama inavyo sema  hii tawaondolea migogoro kwani vikao ndio suluhisho la matatizo katika umoja wao,  
Pamoja na hayo amewataka wenyeviti wa  kata kufanya ziara mara kwa mara  ili kuelimisha kuhusu  kinachofanyika katika serikali yao  hali itaweza kuwafanya  wanachama kutambua umuhimu wao katika nchi yao,bibi mariam asema’’ bila ziara na kufanya vikao kuwafuata wananchi  walipo hatuta jenga umoja wetu wa wanawake “ 
kwa upande mwingine omeongelea kuhusu kuazisha mirada ya chama  amesema wanawake waombe mashamba, viwanja na miradi mingine ili waweza kuendesha chama na kujinua wanawakwe kiuchumi katika mkoa wa mbeya na wanawake wote Tanzania  kwa ujumla pia amewasa wanawake   kujiamini na kujiunga na taasisi za kifadha  au kuanzisha   saccos,au banki ili ziweze kusadia na familia zao hii itawajengea kuijimalisha kifamilia,kijamii na kiuchumi pia
Bibi mariam  ameowamba  madiwani wanawake wanatakiwa   kuwawakilisha wanawake wote Tanzania, na kazi kubwa ni kutekeleza ilani  ya chama cha mapinduzi kwa  kufanya mikutano kwa  kuwaelekeza kitugani serikali ya chama cha mapinzuzi kilichofanya nahii itasaidia wananchi kutambua wajibu wao,madiwani wanakazi kubwa sana ya kuelimisha wananchi wa kata zao
Pia madiwani wa viti maalum kuwaelimiasha wanachama kuhusu ulipaji wa ada ambyo nishilingi 1200 kwa mwanachama mmoja kwa mwaka ,  kwa kuwa madiwa ni wana ushawishi mkubwa sana kwa wanachama wao

Bibi mariam amesama kuwa yuko tayari kufanya kazi na wanawake  wa mkoa  wambeya  na Tanzania  kwa ujumla  kwa  kushikiana na wanawake  wamikoa mingine ya  tanzania
Naye katibu wa uwt wilaya ya mbeya mjini bibi SIFA AMIDU ALIMASI amesema kuwa amefurahi kutembelewa na katibu mpya katika wilaya ya mbeya na wanamkaribisha  kwa mikono miwili na wapo tayari kushirikiana naye ili waeweze kufikisha mipango na malengo  ya umoja huo wa uwt,pamoja na hayo bibi sifa amidu asema  kuwa malengo makubwa ya UWT ni kuwainuwa wanawake kiuchumi na kuwatangezea mazingira mazuri ya kujiamini katika utandaji wa kazi zao na kutatua matatizo na migogoro ya hapa na napale, pia amewataka wanawake wote wa wilaya  ya mbeya na mkoa kwa ujumla kujiunga na umoja huo ili kujikwamua kichumi  
 Bibi sifa Omeongeza kuwa  wanawake kupendane na kuungana mikono husasana   katika kipindi cha uchaguzi ili kuweza kufikisha hasilimia hamsi kwa hamisi,  wanawake wawe  na wivu wamaendeleo na kuondoa kuchafuana  wenyewe kwa wenyewe
  Kwa upande wake mwenyekiti wa wanawake  madiwani wa viti maluum  mbeya mjini bibi AGNESS MANGASILA  asema kuwa wameupokea  wito wa  katibu wa uwt mkoa na kuahidi kuwa madiwani wata fanya kazi kwa kufanya vikao na mikitano ya mara kwa mara  kwa wananchi wao  ili kuelimisha kuhusu serikali yao 

0 comments: