Tuesday 20 May 2014

KAMA HAUJAONA MAJINA NA UTARATBU WA KUJIUNGA NA JKT 2014 KWA WAHITIMU KIDATO CHA VI NI HAYA HAPA

 

UTARATIBU WA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA VIJANA KWA MUJIBU WA SHERIA WANAOMALIZA KIDATO CHA SITA MEI 2014.


  • AWAMU YA KWANZA; Vijana 20,000 wataripoti kwenye makambi ya mafunzo ya JKT kuanzia tarehe 01 Juni 2014 na kuanza rasmi mafunzo yao tarehe 08 Juni 2014 na kumaliza tarehe 04 Septemba 2014. Orodha yao itaanza kuonekana kwenye website ya JKT tarehe 11 Mei 2014 kuanzia saa nne (4) asubuhi. 
  • AWAMU YA PILI; Vijana 14,450 wataripoti kwenye makambi ya mafunzo ya JKT kuanzia tarehe 11 Septemba 2014 na kuanza rasmi mafunzo tarehe 18 Septemba 2014 na kumaliza tarehe 17 Desemba 2014. Orodha yao itaanza kuonekana kwenye website ya JKT tarehe 15 Mei 2014 kuanzia saa kumi (10) jioni.
  • Kijana yeyote mwenye ulemavu unaoonekana aripoiti katika kambi ya mafunzo ya Ruvu JKT (832 Kikosi cha Jeshi).
  • Vijana wote wanatakiwa kuwa na vyeti vya kumaliza Kidato cha Sita (Leaving Certificate).
  • Inasisitizwa vijana waripoti kwenye makambi waliyopangiwa na siyo kuja Makao Makuu ya JKT.
Bofya majina ya makambi yaliyopachikwa hapo chini kupakua na kufungua ukurasa kuona majina ya walioitwa katika Awamu ya Kwanza.
  1. BULOMBORA - KIGOMA
  2. RWAMKOMA - MUSOMA
  3. MSANGE - TABORA
  4. KANEMBWA - KIGOMA
  5. RUVU - PWANI
  6. OLIJORO - ARUSHA
  7. MGAMBO KABUKU - TANGA
  8. MARAMBA - TANGA
  9. MAFINGA - IRINGA
  10. MLALE - SONGEA
  11. MTABILA - KIGOMA
  12. MAKUTOPORA - DODOMA

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana na info@jkt.go.tz

Taarifa hii imetolewa na:
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa.

0 comments: