KISA CHA EMMA ROBERTS NA SHERIA INAYOONGOZA ELIMU TANZANIA
Kupitia kipindi cha Wanawake Live kinachorushwa na EATV kila siku ya Jumanne saa tatu usiku, umma wa Watanzania walipata kufahamu kilichomkuta binti Emma Roberts.
Kwa kukumbusha tu, Emma ni binti aliyefukuzwa shule kutokana na ujauzito. Ujauzito wa Emma ulikuja baada ya kufanyiwa kitendo cha ukatili cha ubakwaji. Kwa mdomo wake mwenyewe, Emma ameelezea hali halisi na kusema kwamba hakupenda huo ndio uwe mustakabali wake wa maisha kwa kuwa alikuwa na ndoto nyingi sana katika maisha. Emma hakupenda

kubakwa. Tukio
hilo limemkosesha nafasi ya kupata haki yake ya msingi, elimu. Emma
katika maelezo yake anasema elimu ndio ingemsaidia katika maisha yake
yeye na mwanae. Akiwa na namba yake ya mtihani tayari kwa ajili ya
kufanya mtihani wa kidato cha nne 2013, Emma alisubiria kwa hamu majibu
ya ombi lake kwa Wizara ya Elimu imruhusu kufanya mtihani huo. Hata
hivyo, Emma hakuweza tena kufanya mtihani kwa kuwa hakupewa ruhusa ya
kufanya hivyo.
Kupitia Wanawake Live, Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Mathias Chikawe amezungumza na kueleza sheria ikoje katika masuala kama haya, na kumalizia kuwa 'Hakuna mimba za bahati mbaya'.

Maswali
ambayo wengi wanajiuliza ni pamoja na Je, sheria inayotumika kuongoza
elimu nchini Tanzania, inawanufaisha wananchi au ni sheria iliyowekwa
kukandamiza kikundi fulani cha watu? Je, Emma Roberts hakupaswa
kupigania haki yake ya kupata elimu eti kwa sababu Mhe Waziri wa Sheria
na Katiba amesema kwamba 'Hakuna mimba za bahati mbaya'?
Mara zote jamii imeshuhudia wasichana wadogo wakifukuzwa shule kutokana na tatizo la mimba, bila kutazama chanzo cha mwanafunzi huyo kupata hiyo mimba. Pia, wahusika wakuu wa mimba hizo (wanaume) wengi wamethibitika kuendelea kupeta tu mtaani bila kuchukuliwa hatua zozote ilhali msichana anakuwa ameshafukuzwa shule na kunyimwa haki yake ya kimsingi.
Muda umefika sasa wanawake kupigania haki zao dhidi ya sheria kandamizi ambazo zinawanyima fursa muhimu katika maisha. Pia, mawazo mgando kama ya Mhe. Chikawe eti 'hakuna mimba za bahati mbaya' ni kitu kinachopaswa kupigwa vita vikali.

habari hii kwa hisani ya wanawakelivetv.com
0 comments:
Post a Comment