Ni
zaidi ya mwaka mmoja umepita toka kufariki kwa mwigizaji staa wa
Tanzania Steven Kanumba, ambae aliacha kampuni ya kutengeneza filamu
aliyokua akiimiliki pamoja na mali nyingine yakiwemo magari.
Baba
mzazi wa Marehemu Mzee Kanumba anaeishi Shinyanga amesema ‘kwenye
mirathi tumeshirikiana na Mama Kanumba ingawa Jaji kachanganya baada ya
kuwekwa watoto ambao sio wangu… mimi na mama Kanumba ni sahihi ila
watoto ambao sio wangu tumeandaa Mwanasheria kuwaondoa wasiohusika na
tumbo langu vinginevyo na wa tumbo langu waingie kwenye mgao wa mirathi’
‘Watoto
walioshirikishwa na sio wangu ni Seth Bosco ambae ni mtoto wa shemeji
yangu mdogo wake mama Kanumba, Tina Mshumbuzi, Bella Kajumulo yani haya
majina unayaona yako tofauti, hawa wawili nilikuta Mama Kanumba
ameshazaa.. kwa hiyo hawawezi kuingia kwenye kurithi ndio maana
nafatilia Mahakama itende haki na watoto wangu waingie mule vinginevyo
aisee patachimbika’ – Baba Kanumba
Kwenye
sentensi ya mwisho Baba Kanumba amesema ‘Kanumba hakua na mke wala
mtoto hivyo hawezi kuingia mwingine pale, mirathi ni ya watu wawili mimi
na Mama Kanumba tuliemleta duniani Kanumba, sijawasiliana bado na Mama
Kanumba…. tutawasiliana Mahakamani’
Baba
Kanumba ambae hakuweza kuhudhuria maziko Dar es salaam kutokana na
kuumwa, anasema kwenye mazungumzo ya mwisho na Marehemu siku kadhaa
kabla ya kufariki, alimwambia kuhusu pesa zaidi ya milioni 50 alizokua
nazo benki pamoja na nyumba aliyokua ameianza ujenzi Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment