1954-HUNGARY
4 URUGUAY 2.
Hii
ndio nusu fainali inayosemwa kuwa kubwa zaidi katika michezo ya nusu fainali za
kombe la dunia. Hungary iliyoiharibu Ujerumani Magharibi kwa mabao 8-3 katika
mchezo wa makundi, iliongoza kwa mabao 2-0 dhidi ya mabingwa watetezi Uruguay mpaka
dakika za mwisho na kuonekana inatinga fainali.
Lakini
taifa hilo la Amerika kusini lilipambana kupitia kwa Juan Hohlberg aliyefunga
mabao mawili na kuipeleka mechi katika dakika za nyongeza.
Mabao mawili ya kichwa kupitia kwa Sandor
Kocsic, aliyefunga mara 11 katika mashindano yote, yaliipa Hungary ushindi wa
mabao 4-2. “Ilikuwa nusu fainali nzuri mno, ilikuwa mechi ya kasi, ufundi kwa
timu zote”. Alisema nyota wa Hungary, Jozsek Boszik. Lakini walipoteza tena kwa
mabao 3-2 dhidi ya Ujerumani Magharibi katika mechi ya fainali.
1966-
ENGLAND 2 PORTUGAL 1
Ureno
wakijivunia zaidi nyota wao mkali `Black
Panther` Eusebio katika fainali hizo walipoteza mchezo dhidi ya England. Mabao
mawili ya Bobby Charlton yaliwafanya wenyeji waongoze kwa mabao 2-0 mpaka
dakika 10 za mwisho.
Eusebio,
aliyenyimwa nafasi za kufunga na kipa wa England, Gordon Banks kwa muda wote wa
mchezo, alipata penati dakika ya 83 na kufunga. Hili lilikuwa bao la kwanza kwa
England kufungwa katika mashindano hayo.
Licha
ya kupata presha katika dakika za mwisho, England walifuzu fainali. “Kile
kilikuwa kiwango kikubwa zaidi walichoonesha England mpaka leo hii,” alisema
kocha Alf Ramsey. Wakati mpinzani wake, kocha wa Ureno, Otto Gloria alisema
England itaifunga Ujerumani katika mchezo wa fainali kama itacheza soka kama
lile. Ujerumani walitegemea sana soka la nguvu”. Alisema.
1970-ITALIA
4 UJERUMANI MAGHARIBI 3
Ukikumbuka
mchezo huu wa karne ya 20, Italia walipata bao la kuongoza dakika nane tu za
mchezo kupitia kwa Roberto Boninsegne na waliamua `kupaki` basi mpaka dakika ya
mwisho ambapo Uwe Seeler alisawazisha.
Bao
hilo liliupeleka mchezo katika dakika za nyongeza. Gerd `Der Bomber` Muller
aliifungia Ujerumani bao la kuongoza, lakini Italia wakasawazisha, kabla ya
kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Luigi Riva.
Muller
alifunga tena, lakini wakati Wajerumani wakiendelea kufurahia bao hilo, Italia
walifunga bao la nne kupitia kwa Gianni Rivera na bao hilo likamaliza mchezo. Italia
walicheza mpira mkubwa dhidi ya Brazil katika mchezo wa fainali, lakini
walipoteza kwa mabao 4-1.
1980-UJERUMANI
MAGHARIBI 3 UFARANSA 3 ( UJERUMANI WALISHINDA KWA PENATI 5-4).
Ilikuwa
mechi ya maajabu. Ujerumani walifunga bao la kuongoza kupitia kwa Pierre
Littbarski. Lakini Ufaransa walisawazisha kwa penati kupitia kwa Michel
Platini. Muda wa nyongeza Ufaransa walifunga mabao mawili kupitia kwa Marius
Tresor na Alain Giresse. Hata hivyo, Ujerumani walisawazisha na kuwa 3-3
kupitia kwa Karl-Heinz Rummenigge na Klaus Fischer. Maxime Bossis alikosa
penati iliyookolewa na kipa Schumacher na Ujerumani kushinda kwa penati 5-4.
Ufaransa walikuwa wabunifu, lakini Ujerumani walikuwa na nguvu.
1998-UFARANSA
2 CROATIA 1.
Wenyeji Ufaransa walikosolewa sana mpaka kufika hatua ya nusu fainali. Croatia wakishiriki fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza baada kujitenga na Yugoskavia, walifunga bao la kuongoza dakika moja tu baada ya kipindi cha pili kuanza kupitia kwa Davor Suker. Hata hivyo, Ufaransa walisawazisha dakika moja baadaye kupitia kwa beki wake Lilian Thuram, hilo likiwa bao lake la kwanza katika soka la kimataifa. Thuram pia alifunga bao la pili, alipiga magoti na kushangilia sana. Kitu pekee cha huzuni katika mechi ile ilikuwa ni kitendo cha Slaven Bilic kupigwa kichwa na Laurent Blanc na kusababisha Blanc apate kadi nyekundu. Alikosa mechi ya fainali ambayo Ufaransa walishinda mabao 3-0 dhidi ya Brazil.
0 comments:
Post a Comment