NAHODHA wa zamani wa Ujerumani, Lothar Matthaus
anaamini Pep Guardioala ameingiza sumu zake kwenye timu ya taifa kwasababu kuna
wachezaji wengi wa Bayern Munich.
Kocha huyo wa zamani wa Barcelona alianza kazi
Bayern tangu majira ya kiangazi mwaka 2013 na kuiongoza klabu hiyo kutwaa
makombe mawili ya nyumbani katika msimu wake wa kwanza.
Matthaus anaamini falsafa ya mpira wa Hispania
imeingia katika wachezaji na kuanza kufanya kazi kwenye timu ya taifa wakitokea
katika klabu yao ya Bayern Munich.
“Ni kweli kwamba Guardiola amekuwa na ushawashi
fulani katika timu yetu. Inahusisha wachezaji wengi wa Bayern na wameanza
kuleta staili yao ya mpira”. Alisema.
“Guardiola alishinda mataji mengi sana akiwa
Barcelona na alikuwa na mafanikio makubwa. Alichukua baadhi ya falsafa za
Barcelona na kuja nazo Bayern, na kwa vile Ujerumani ina wachezaji wengi wa
Bayern, kumekuwepo na elementi za Guardiola katika timu”.
Matthaus alibeba kombe la dunia akiwa nahodha
mwaka 1990- na mpaka sasa hakuna nahodha yeyote wa Ujerumani aliyefanikifiwa
kupata mafanikio hayo.
Pia anashikilia rekodi ya kucheza mechi nyingi
za kombe la dunia akiwa alicheza mechi 25.
Japokuwa
kikosi cha Joachim Low kinajulikana kwa kucheza soka la kuvutia,
Matthaus amekiri kuwa timu hiyo kwasasa imebadilika na kucheza mpira wa nguvu utakaowasaidia
kupata mafanikio katika fainali yao ya nne mfululizo ya kombe la dunia.
“Kushinda ndio kitu cha msingi zaidi katika
fainali za kombe la dunia. Tumetumia miaka nane kucheza soka la mvuto, soka la
ufundi, kwa staili ambayo hakuna aliyeijua Ujerumani na ilipokelewa vizuri,”
Matthaus alisema.
“Kwasasa kuna mabadiliko yaliyoondoa uzuri wa soka letu, lakini tunaangalia zaidi
kushinda”.
“Katika fainali za Afrika kusini, Ujerumani
iliwashangaza wengi kwa soka lao zuri. Hapa Brazil wanacheza soka kwa nguvu,
wanatafuta matokeo zaidi”.
Kesho Ujerumani inacheza nusu fainali ya kwanza
ya kombe la dunia dhidi ya Wenyeji Brazil na keshokutwa, Uholanzi watachuana na
Argentina.
0 comments:
Post a Comment