CESARE Prandelli amethibitishwa kuwa kocha mkuu wa
klabu ya Galatasaray ya Uturuki zikiwa zimepita wiki mbili tangu ajiuzulu
kuifundisha timu ya Taifa ya Italia kutokana na matokeo mabaya ya kombe la
dunia nchini Brazil.
Miamba hiyo ya Uturuki imeweka taarifa rasmi kwenye
mtandao wao wa klabu leo jumatatu, ikisema kuwa kocha huyo mwenye miaka 56 atasaini
mkataba wa miaka miwili kurithi mikoba ya Roberto Mancini.
Prandelli atawasili Uturuki leo jioni kabla ya
kusaini mkataba, na kesho jumanne
atatembelea uwanja wa mazeozi pamoja na wachezaji.
Galatasaray walikuwa wakihusishwa kuzungumza na
Prandelli tangu ajiuzulu kuifundisha Italia, huku David Moyes naye akihusishwa.
Prandelli atamrithi Mancini katika dimba la Turk
Telekom Arena kufuatia kocha huyo kuondoka kwa makubaliano maalum mwezi juni
ikiwa ni miezi tisa tangu aanze kazi hiyo.
Mkurugenzi wa michezo wa Galatasaray, Tomas
Ujfalusi, siku za karibuni alikiri kuwa ujuzi na uzoefu wa Prandelli katika
soka la Italia utasaidia kuendeleza kazi aliyofanya Mancini klabuni hapo.
“Wakati Mancini anasema hataki kuendelea, nilataka kumleya Cesare,” Ujfalusi alikaririwa akizungumza na gazeti la Gazetta dello Sport.
0 comments:
Post a Comment