Mhe. Gaudentia Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira akipata
ufafanuzi kuhusu mpango wa uchangiaji wa Wakulima na wachimbaji wadogo wa
madini kutoka kwa Meneja Kiongozi Uhusiano na huduma kwa wateja Mrs Eunice
Chiume wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea Banda la
Shirika hilo katika Maonyesho ya 38 ya Kibiashara (Sabasaba)
ufafanuzi kuhusu mpango wa uchangiaji wa Wakulima na wachimbaji wadogo wa
madini kutoka kwa Meneja Kiongozi Uhusiano na huduma kwa wateja Mrs Eunice
Chiume wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea Banda la
Shirika hilo katika Maonyesho ya 38 ya Kibiashara (Sabasaba)
Mh.Gaudentia
Kabaka, Waziri wa Kazi na Ajira akipata maelezo kuhusa mradi wa DEGE
ECO VILLAGE kutoka kwa Mhandisi Julius Nyamuhokya wa Shirika la Taifa la
Hifadhi ya Jamii (NSSF) alipotembelea Banda la Shirika hilo leo katika
Maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Meneja Kiongozi, Uhusiano na Huduma kwa
wateja wa NSSF Mrs Eunice Chiume.
MAMIA WAJITOKEZA KUSHUHUDIA NA KUPATA UKWELI JUU YA MCHANGA WA DHAHABU
Watumishi wa TMAA wakiwa tayari kuwaelimisha na kuwahudumia wananchi waliotembelea Banda lao kwenye viwanja vya Saba Saba.
Baadhi ya wananchi waliotembelea Banda la TMAA wakishuhudia mchanga wa dhahabu uliokuwa ukioneshwa banda hapo.
Picha zote na Saidi Mkabakuli
…………………………………………………………
Na Saidi Mkabakuli
Mamia
ya wakazi ya jiji la Dar es Salaam na vitongoji vya wamejitokeza
kujionea mchanga wa dhahabu unaoneshwa kwenye Banda la Wakala wa Ukaguzi
wa Madini Tanzania (TMAA) lililopo katika viwanja vya Maonesho ya
Kimataifa vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa wakazi hao Bw. Shabaan Charahani, amesema ameshawishika kuja
kujionea mchanga huo na kupata ukweli juu ya kutoroshwa kwa mchanga huo
kama inavyovumishwa na watu wengi nchini.
“Nimekuja
kujifunza masuala ya ukaguzi wa madini na kujua ukweli juu ya mchanga
wa dhahabu unaozalishwa hapa nchini,” alisema Bw. Charahani.
Akitoa
maelezo kwa wananchi hao waliojitokeza bandani hapo, Afisa Habari wa
Wakala huo, Mhandisi Yisambi Shiwa alisema kuwa mchanga wa dhahabu ni
zao lenye madini ya shaba na fedha lipatikanalo mara baada ya kuchenjua
mawe yenye dhahabu kwenye mtambo wa kuchenjulia mawe hayo uliopo kwenye
migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi.
Aliongeza
kuwa kuna mkanganyiko wa matumizi sahihi ya neno mchanga wa dhahabu,
ambapo kiusahihi mchanga wa dhahabu ni makinikia ya shaba (copper
concentrate).
“Kutokana
na madini ya shaba kuwa mengi kwenye huu ‘mchanga wa dhahabu’ kuliko
madini mengine, jina rasmi linalotumika na kutambulisha zao hili ni
makinikia ya shaba,” alifafanua.
Kwa
mujibu wa Mhandisi Shiwa, kwa sasa, uzalishaji wa makinikia ya shaba
unafanyika katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi tu. Akiitaja sababu ya
kuwepo na aina ya mashapo ya dhahabu ya migodi hiyo kuwa na sifa
tofauti na migodi mingine mikubwa ya dhahabu hapa nchini.
Akitaja
sababu za kusafirishwa nje ya nchi mchanga huo, Mhandisi Shiwa kwamba
kutokuwepo kwa teknolojia ya kutenganisha madini hayo, pamoja na gharama
kubwa za kuendeshea mtambo wa kufanya kazi hiyo.
“Gharama
za mtambo wa kuchenjulia madini hayo ni wastani wa dola za kimarekani
milioni 500. Gharama hizi ni kubwa ukilinganisha na hali halisi ya
mapato ya migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi yatokanayo na ‘mchanga wa
dhahabu’,” alisema Mhandisi Shiwa.
Mhandisi
Shiwa aliongeza, “kutokuwepo na umeme wa uhakika na uzalishaji duni wa
makinikia hayo ndo sababu kuu za kutofanyika kwa kazi hiyo hapa nchini,”
aliongeza.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizopo kiasi cha makinikia kinachozalishwa hapa
nchini ni wastani wa tani 45,000 ilhal kiasi kinachotakiwa ni wastani wa
tani 150,000 za makinikia ya shaba.
TMAA
ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini ya
Sheria ya Wakala wa Serikali, Sura ya 245. Tamko la Waziri la kuanzisha
Wakala lilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 362 la tarehe 6
Novemba, 2009. Lengo la Wakala ni kuhakikisha kwamba, Serikali inapata
mapato stahiki kutoka kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya
madini nchini kupitia usimamizi na ukaguzi makini wa shughuli za
uchimbaji, na kuhakikisha kuwa shughuli hizo zinafanyika kwa kuzingatia
uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika maeneo ya migodi.
0 comments:
Post a Comment