NAHODHA wa zamani wa England, David Beckham anatabiri
kumuona Lionel Messi akifanya maajabu katika fainali ya kombe la dunia
na kuiongoza Argentina kutwaa ubingwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka
1986.
Messi anakosolewa na wadau wa
soka kwamba ameshindwa kuonesha kiwango chake cha Barcelona katika soka
la kimataifa, lakini amefanya kazi kubwa kuifikisha Argentina katika
fainali ya leo usiku dhidi ya Ujerumani.
“Ni mtu wa ajabu,” Beckham alisema kwenye mahojiano na chaneli ya Adidas football ya YouTube.
“Amepata uwezo
binafsi mkubwa, lakini ushindi unamaanisha kila kitu kwake. Kama
wachezaji wenzake wanafunga mabao, anakuwa wa kwanza kushangilia nao na
nadhani ile ina maana kubwa kuhusu yeye”
“Kucheza na
Argentina, nina uhakika kuna presha kiasi fulani ukiangalia huko
walikotoka. Kushinda ina maana kubwa kwake, familia na kila mmoja
anayemzunguka duniani”.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment