Sunday, 13 July 2014

VAN GAAL: TUMEONESHA JINSI GANI SISI NI BORA, AJABU TUMETUMIA WACHEZAJI WOTE 23

434669_heroaUHOLANZI imeonesha ubora wake kwa kuipiga Brazil mabao 3-0 jana usiku na kutwaa nafasi ya tatu ya kombe la dunia, kwa mujibu wa kocha Louis van Gaal.
The Orange ilipata ushindi mnono dhidi ya wenyeji na shukurani kwa mabao ya Robin Van Persie, Daley Blind na Georginio Wijnaldum, ambapo ilikuwa mechi ya mwisho kwa Van Gaal kuiongozo Uholanzi kabla ya kuanza kazi mpya katika klabu ya Manchester United.
Kocha huyo alisema alikuwa na furaha kuona wachezaji wake wameimarika vizuri kufuatia kufungwa na Argentina katika mchezo wa nusu fainali.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.blospot.com

Related Posts:

0 comments: