LUIZ
Felipe Scolari amesema hatajiuzulu katika nafasi yake ya ukocha wa timu
ya taifa ya Brazil, licha ya timu yake kufungwa mara ya pili mfululizo
ndani ya siku tano.
Brazil walifungwa mabao 7-1 katika
mechi ya nusu fainali iliyopigwa Belo Horizonte siku ya jumanne ya wiki
hii na usiku wa jana walifungwa mabao 3-0 na Uholanzi na kumaliza
katika nafasi ya nne ya fainali za 2014 za kombe la dunia kwenye ardhi
yake.
Kabla ya mashindano haya, Brazil
ilikuwa haijapoteza mechi nyingi za nyumbanii tangu mwaka 2002 na
walikuwa hawajawahi kufungwa nyumbani katika mashindo ya mpira wa miguu
tangu mwaka 1975, lakini kufungwa mara mbili mfululizo ndani ya siku
tano kumewachangaya mashabiki na waandishi wa habari wan chi hiyo.
Kusoma zaidi bofya www.bkmtata.bloggspot.com
0 comments:
Post a Comment