Rais Jakaya Kikwete akiongoza Kikao
cha Ujumbe wa Mawaziri na Wakuu wa Taasisi za Uhifadhi nchini kabla ya
kuanza rasmi kwa Mkutano wa Kimataifa wa Kuzuia Biashara Haramu ya
Wanyamapori jijini London, Uingereza.
Mkutano wa Kimataifa kuhusu Biashara
Haramu ya Wanyamapori (Conference on Illegal Wildlife Trade) unaanza
rasmi leo katika ukumbi wa Lancaster House.
Mkutano huu utakaohudhuriwa na jumla
ya mataifa 47 na Mashirika 13 ya Kimataifa umeitishwa na Serikali ya
Uingereza kwa lengo la kujadiliwa na masuala maalum matatu kuhusiana na
biashara haramu ya wanyamapori. Masuala maalum uyanayotarajiwa
kujadiliwa ni Jinsi ya Kuimarisha Usimamizi wa Sheria (Law Enforcement)
na mchango wa mfumo mzima wa sheria za jinai (criminal justice system)
katika kukabiliana na biashara hiyo.
Aidha, utajadili Jinsi ya kupunguza
hitaji la bidhaa zinazotokana na wanyamapori (demand for wildlife
products) na Jinsi ya kusaidia Maendeleo Endelevu kwa Jamii
zilizoathiriwa na biashara hiyo haramu.
Mkutano huu utazungumzia wanyama aina
ya tembo, faru na tiger. Wanyama hawa wamechaguliwa kwa kuzingatia jinsi
wanavyoshambuliwa zaidi na makundi ya wawindaji haramu kwa lengo la kuu
pembe na ngozi zao.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete tayari
ameshawasili Uingereza akiongoza ujumbe wa maafisa kutoka Serikali ya
Tanzania kwa ajili ya kushiriki Mkutano huu.
0 comments:
Post a Comment