UWANJA: HARRAS EL-HEDOUD STADIUM, ALEXANDRIA, MISRI
>>TANZANIA HAINA TENA MWAKILISHI AFRIKA!
MABINGWA
wa Tanzania Bara, Yanga, Usiku huu wameyaaga Mashindano ya Afrika ya
CAF CHAMPIONZ LIGI baada kutolewa na Mabingwa Watetezi wa Afrika, Al
Ahly, kwa Penati 4-3.
Kwenye Mechi ya Usiku huu iliyochezwa
bila Watazamaji ndani ya Uwanja Harras El-Hedoud Mjini Alexandria,
Nchini Misri, Al Ahly walishinda Bao 1-0, kwa Bao la Dakika ya 71 la
Sayed Moawad, na hivyo kuipeleka Mechi kwenye Tombola ya Penati kwa vile
Yanga walishinda Mechi ya Kwanza Jijini Dar es Salaama Bao 1-0.
Penati za Yanga zilifungwa na Didier
Kavumbagu, Nadir Haroub ‘Canavaro’, Emmanuel Okwi na waliokosa ni
Oscar, Said Bahanuzi na Mbuyu Twite huku pia Kipa Deo Munish akiokoa
Penati mbili.
Matokeo haya yameiacha Tanzania bila
Klabu yeyote kwenye Michuano ya Afrika baada ya Klabu nyingi 3, Azam FC,
KMKM na Chuoni, kutolewa nje Raundi iliyopita kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI
NA Kombe la Shirikisho.
Sasa Al Ahly wanatinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na watacheza na Al Ahli - Benghazi ya Libya.
VIKOSI:
ALA AHLY: Sherif
Ekramy, Saad Samir, Mohamed Naguib, Ahmed Fathi, Sayed Moawad, Rami
Rabia, Hossam Ashour,Abdallah El-Said, Moussa Yedan, Gedo, Amr Gamal
YANGA: Deo Munish
"Dida", Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin
Yondani "Cotton" , Frank Domayo "Chumvi", Saimon Msuva, Mrisho Ngasa,
Didier Kavumbagu, Emmanuel Okwi, Hamisi Kizza
Akiba: Kaseja, Juma, Luhende, Athuman Iddi "Chuji", Nizar Halfan, Said Bahanuzi , Jerry Tegete
Refa: Badara Diatta [Senegal]
CAF CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Kwanza
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao Mechi mbili/Matokeo Mechi za Kwanza]
Ijumaa Machi 7
Kabuscorp – Angola 0 Al Zamalek – Egypt 0 [0-1]
Jumamosi Machi 8
Kampala City Council FC – Uganda 1 Nkana FC – Zambia 2 [3-4]
Coton Sport FC – Cameroon 5 Flambeau de l’Est – Burundi 0 [5-0]
ASFA-Yennenga - Burkina Faso 0 Entente Sportive de Sétif – Algeria 0 [0-5]
Liga Muculmana de Maputo – Mozambique 0 Kaizer Chiefs - South Africa 3 [0-7] Primeiro de Agosto – Angola 2 AC Leopards de Dolisie – Congo 0 [3-4]
AS Bamako – Mali 0 Enyimba International FC – Nigeria 1 [2-2]
Raja Club Athletic – Morocco 1 Horoya Athlétique Club – Guinea 0 [0-1, Penati 4-5]
Jumapili Machi 9
Al Ahly – Egypt 1 Young Africans – Tanzania 0 [1-1, Penati 4-3]
Al Ahli - Benghazi – Libya 2 Berekum Chelsea - Ghana 0 [3-1]
TP Mazembe - Congo, DR 3 Les Astres de Douala – Cameroon 0 [4-1]
AS Vita Club - Congo, DR 1 Dynamos – Zimbabwe 0 [1-0]
Espérance Sportive de Tunis – Tunisia v Gor Mahia – Kenya [3-2]
Sewe Sport - Ivory Coast v Barrack Y.C.II – Liberia [3-3]
Al-Hilal – Sudan v Stade Malien de Bamako – Mali [0-0]
Club Sportif Sfaxien – Tunisia 2 Dededbi – Ethiopia t 0 [4-1]
0 comments:
Post a Comment