- Inter wanataka Fernando Torres aungane na Nemanja Vidic, ambaye amekubali kujiunga na klabu hiyo ya Italia baada ya kumalizika kwa mkata wake na Manchester United mwishoni mwa msimu huu.
- Chelsea wanatarajia kuiwania saini ya nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa, nyota wa Monaco, Radamel Falcao na mtukutu wa AC Milan, Mario Balotelli
- Chelsea wanataka kutumia dau kubwa zaidi kusajili majira ya kiangazi, lakini wanahitaji kuuza wachezaji ili kuendana na sheria ya matumizi ya fedha ya UEFA (UEFA’s Financial Fair Play restrictions).
KLABU
ya Inter Milan imeandaa kitita cha paundi milioni 20 kuinasa saini ya
mshambuliaji wa Chelsea, Raia wa Hispania, Fernando Torres ambaye mpaka
sasa anashikilia rekodi ya uhamisho nchini England.
Torres amebakisha miaka miwili katika mkataba wake ambao analipwa pauni laki moja moja na nusu kwa wiki.
Nyota
huyo alijiunga na Chelsea akitokea Liverpool miaka mitatu iliyopita kwa
ada ya uhamisho wa paundi milioni 50, lakini sasa inaoneakana anaweza
kuuzwa kutokana na kocha wake Jose Mourinho kuhitaji kutumia fedha
nyingi kufanya usajili msimu ujao.
Diego
Costa, Radamel Falcao na Mario Balotelli ndio chaguo la Mourinho,
lakini Chelsea wanahitaji kuwa makini ili kutovunja sheria ya matumizi
ya fedha ya UEFA.
Katika
biashara hiyo, Torres ndiye atakayeamua kitita cha kulipwa hata kama
thamani yake imeshuka kufuatia kuwa katika kiwango cha chini miaka yote
mitatu darajani.
Mmiliki
mpya wa Inter, mfanya biashara Raia wa Indonesia, Erick Thohir
amesisitiza kuwa hatatumia pesa nyingi kujenga timu, lakini atatoa fedha
kiasi ili kumuunga mkono kocha wake Walter Mazzarri katika msimu wa
usajili.
Wawakilishi
wa Inter walikuwa katika mzungumzo na Chelsea kipindi cha usajili wa
dirisha dogo wakimuomba Juan Mata ili wabadilishane na Fredy Guarin.
Lakini hakuna dili lililokamilika na b, hivyo klabu hiyo ya Italia
inarudi kwa Torres.
Hali ngumu: Torres amekuwa katika wakati mgumu sana tangu asajiliwe na Chelsea akitokea Liverpool kwa ada ya paundi milioni 50
Jembe jipya!: Jose Mourinho ametaja wachezaji anaowania akiwemo nyota wa Atletico Madrid, Diego Costa
Mtukutu: Mourinho anataka kuungana na mshambuliaji wa zamani wa Inter Milian na sasa akiichezea AC Milan, Mario Balotelli,
Usajili
wa Torres unakuja baada ya Iinter kutangaza kumsajili nahodha wa
Manchester United Nemanja Vidic kwa ajili ya msimu ujao.
Mtandao wa Sportsmail uliweka
wazi siku za nyuma jinsi ambavyo Inter wanahitaji kumsajili beki huyo
mkongwe wa Man Unted ambaye aliweka bayana kuwa anataka kuondoka
mwishoni mwa msimu.
Klabu
ya Inter imethibitisha kukamilisha usajili wa Vidic jumanne ya wiki hii
na picha ya mkongwe huyo iliwekwa katika mtandao rasmi wa Twita wa
Inter na kuandikiwa maneno ya kumkaribisha ambayo yalisomeka; ” Hapa
Vidic anasaini mkataba wake. Tutaonana mwezi wa sita, Nemanja!”
Makubaliano yameshafikiwa katika mkataba huo wa miaka miatatu ambao utampeleka Vidic katika kustaafu soka.
Anasepa zake!: Vidic atajiunga na Inter baada ya kumalizika kwa mkataba wake msimu huu katika klabu yake ya Manchester United
0 comments:
Post a Comment