Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Singida SACP, Geofrey Kamwela.
Na Nathaniel Limu, Singida
MKULIMA mkazi wa kijiji cha Nkalankala kata ya
Mwanga,tarafa ya Nduguti wilaya ya Mkalama mkoani Singida ambaye ni
mlemavu wa ngozi (albino) ,Hidaya Omari (20),anashikiliwa na jeshi la
polisi kwa tuhuma ya kumnyonga hadi kufa, mtoto wake wa kiume mwenye
umri wa mwaka moja na nusu,na kisha kumchuna ngozi katika sehemu yake ya
siri.
Mtoto aliyenyongwa na kuchunwa ngozi ya sehemu yake ya siri na kutupwa kwenye kisima cha maji chenye kina cha mita moja,ni Richard Paulo.
Imedaiwa pia mama
yake mzazi na mtuhumiwa Hidaya,Neema Paulo (35), naye anashikiliwa na
polisi kwa tuhuma ya kuhusika kumnyonga Daudi Richard na kumsababishia
kifo.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoani Singida,SACP,Geofrey Kamwela,alisema tukio
hilo la kusikitisha,limetokea machi 13 mwaka huu saa moja na nusu
asubuhi huko katika kijiji cha Nkalankala wilayani Mkalama.
Alisema mtoto huyo Daudi,aliokotwa akiwa anaelea juu ya maji ya kisima chenye urefu wa mita moja.
Kamwela
alisema uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi,umebaini kuwa Daudi
(marehemu) aliuawa na kuchunwa ngozi yake na kutumbukizwa katika kisima
hicho.
Alisema
mwili wa marehemu ulipofanyiwa uchunguzi na daktari katika eneo la
tukio na kubaini kuwa kabla ya mauaji jhayo,mtoto huyo alinyongwa shingo
yake.Chanzo cha mauaji hayo,inasadikiwa kuwa ni imani ya kishirikina.
Kamanda Kamwela alisema mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa mtu na mama yake,watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili.














Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha
Kwaruhombo,leo Machi 16,2014.Ridhiwani Kikwete ameahidi kuyashughulikia
Matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo Wananchi wote wa Jimbo la
Chalinze,yakiwemo ya Barabara,Maji,Elimu,Matibabu na mengine mengi
ambapo amesema atayafanyia kazi atakapopewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa
Wanachalinze.Picha na Othman Michuzi
- Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wapungua mkono wananchi wa Kijiji cha
Kwarihombo,wakati alipokuwa akiwasili kwenye Kijiji hicho,leo Machi
16,2014.Picha na Othman Michuzi.
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini
Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye
alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea
kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi
kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.Picha na Othman
Michuzi
Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja
wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi
wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha
Chang’ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia
Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze leo
Machi 16,2015.Picha na Othman Michuzi
Mgombea
Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la
Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea Jogoo kutoka kwa kina Mama wa
Kijiji cha Kwamsanja,Kata ya Kibindu leo Machi 16,2914.Picha na Othman
Michuzi 




Wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakisherehekea ushindi jioni hii






















































