‘We Talking Money You Talking Nonsense’ huenda ikawa kauli nzuri kuelezea hiki walichokifanya P-Square kwa sasa.
Hakuna
ubishi kuwa, kwa hiki walichokifanya sasa, na kama macho yetu
hayatudanganyi kwa hiki yanayokiona, mapacha hawa wamefanya kufuru. Kama
hii inayoonekana ni dhahabu kweli, basi P-Square, hela wanayo.
Peter
ameshare picha hizi nne ambazo wiki hii zitakuwa gumzo barani Afrika
ambapo kwenye picha moja inayomuonesha pacha mwezie Paul akiwa amesimama
kwenye sebule mpya inayoaminika kuwa ya nyumba yao mpya, ameandika
‘Goldenworld #blessed.’
Kwenye
picha nyingine, wanaoonekana wakiwa pamoja kwenye sebule hiyo
iliyotawaliwa na kile kinachoonekana kama dhahabu zilizozunguka sofa za
kuvutia na Peter ameandika: #2kings…… Work hard,play harder.’
Picha
nyingine inamuonesha Peter akiwa peke yake kwenye meza ya chakula,
kubwa, iliyojaa vyombo vya thamani vya kuvutia na ameandika: A king in
my own world…. #Blessed.”
Hawa jamaa ni noma.
0 comments:
Post a Comment