![]() |
KIONGERA (KUSHOTO) AKIWA KAZINI |
Mshambuliaji mpya
wa Simba, Modo Kiongera anatarajia kuwasili nchini kesho au keshokutwa ili
kumalizana na uongozi wa klabu hiyo.
“Kiongera
anatarajia kutua nchini kwa ajili ya kusaini mkataba mpya wa miaka miwili na
Simba.
“Mazungumzo
yamekwenda vizuri limebaki suala hilo la mkataba tu,” kilieleza chanzo ndani ya
Simba.
Kamati ya
usajili ya Simba imekuwa ikiendeleza harakati zake za usajili kwa ajili ya
kuboresha kikosi kipya.
Kiongera
aliyewahi kufanya kazi na Kocha Zdrakvo Logarusic anasifika kwa mashuti makali
na mipira ya vichwa.
0 comments:
Post a Comment