Katibu wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoa wa Mbeya, Bashiru Madodi.
Na Mwandishi wetu
Katibu
wa siasa na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), mkoa wa Mbeya, Bashiru
Madodi, amesema kuwa tatizo kubwa la baadhi ya vijana wa chama
hicho(UVCCM), wanatumika vibaya na wagombea na kukisemea chama bila
utaratibu.
Madodi
alisema hayo katika ukumbi wa CCM mkoa wa Mbeya, wakati wa Baraza kuu
la UVCCM Mkoani hapa, ambalo lilifanyika kwa mujibu wa kanuni za umoja
huo kwa ajili ya maandalizi ya kumwapisha kamanda wa Vijana hao mkoa wa
Mbeya, Yona Sonelo na makamanda wa wilaya zote tisa za mkoa huo.
Kauli
ya Madodi imetafsiriwa kama anamjibu Katibu wa hamasa wa UVCCM Taifa,
Paul Makonda, ambaye hivi karibuni ametoa tamko kuwa Waziri Mkuu
aliyejiuzuru, Edward Lowassa kuwa hafai kuwania nafasi ya Rais wa
Tanzania, alisema kuwa inashangaza vijana kuenda mbio na kutoa matamko
ambayo yanapaswa yatolewe na vikao vya chama kwanza.
Alisema
kuwa, vijana wengi wanatembea na wanaotaka madaraka, kutokana na vijana
kuwa ndiyo tegemea la taifa, kwasababu wanaweza kukimbia huku na kule.
“Ni
kipindi kigumu sana kwenu, wakati wetu akina Guninita waliwahi kufutwa
uongozi kutokana na tabia zinazofanana na vijana wa leo. Mnatoa matamko
bila hata vikao vya chama kutoa maamuzi” alisema huku akishangiliwa.
“Makonda
anatakiwa atafsiri vema kauli ya Madodi na kurejea kwenye misingi ya
kanuni ili aweze kufanya vema kazi za jumuiya yake ya watoto badala ya
kila wakati kuinuka na kutoa matamko ambayo yanaashiria yupo na kiongozi
mmoja mfukoni kutafuta nafasi ya Rais mwaka 2015”
Kwa
upande wake, Paul Makonda ambaye alikuwepo kwenye Baraza hilo, ndiye
aliyeanza kueleza kuwa vijana wapo ndani ya mifuko ya wanasiasa wakubwa,
ndiyo maana inafiia mahala chama hakiwaamini.
Alisisitiza
kuwa, kuna baadhi wanaomtuhumu kuwa yeye anatumwa na kundi la watu
kutoa matamko, jambo ambalo siyo la kweli bali anaongozwa na akili zake
mwenyewe na madhara ya magenge ni kujitafutia riziki binafsi.
Mwenyekiti
wa UVCCM Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna, alisema kuwa vijana wangoje chama
kitoe maamuzi kwanza ya mgombea nafasi ya Urais ndipo vijana wamuunge
mkono mtu huyo, badala ya kugawanyika kwa sasa.
Mgeni
rasmi katika ufunguzi wa Baraza hilo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mbeya,
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo chakula na ushirika, Godfrey Zambi,
alisisitiza umoja miongozi mwa Jumuiya hiyo ya vijana kwa maslahi ya
chama na Taifa.
0 comments:
Post a Comment