HOME »
» SIMBA SC WAANZA KUJIFUA KESHO BOKO
KIKOSI
cha Simba ya jijini Dar es Salaam kinatarajia kuanza mazoezi kesho
kwenye Uwanja wa Boko Veteran ulioko Boko kwa ajili ya kujiandaa na
msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara imeelezwa.
Akizungumza
na BIN ZUBEIRY leo mjini Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa Simba,
Selemani Matola, amesema kuwa tayari wachezaji wa timu hiyo wameshapewa
taarifa za kuanza kwa mazoezi hayo tayari kunoa makali kwa msimu mpya wa
ligi. Matola amesema kuwa mazoezi yataanzia gym Chang'ombe na jioni yatakuwa uwanjani.
 |
Suleiman Matola kulia akiwa na bosi wake, Zdravko Logarusic |
Amesema
kuwa licha ya kuchelewa kuanza maandalizi yake, wanaamini wachezaji
watakuwa kwenye kiwango cha juu kutokana na kila mmoja kufanya mazoezi
binafsi.
"Kabla
mwalimu ( Zdravko Logarusic) hajaondoka, aliwaeleza wachezaji wajitunze
na wawe wanafanya mazoezi ili kujiweka tayari na programu alizoziandaa
za msimu mpya," amesema.
Kikosi hiko kinatarajia kuanza mazoezi chini ya Matola, kutokana na Logarusic, kuchelewa kuwasili nchini kama ilivyotarajiwa.
Habari
za ndani zilizopatikana jana mchana zinasema kwamba Mcroatia huyo
atawasili nchini Alhamisi na Ijumaa ataungana na wachezaji wake
kuendelea na mazoezi.
Simba pia inatarajia kuelekea Afrika Kusini kuweka kambi ya siku 17 na itaondoka nchini Julai 20.
Hata
hivyo katika kambi hiyo huenda ikawakosa nyota wake watano walioko
katika timu ya Taifa (Taifa Stars) ambao wanajiandaa kuikabili Msumbiji.
Nyota hao ni pamoja na Ramadhan Singano 'Messi', Amri Kiemba, Jonas Mkude, Joram Mgeveke na Haroun Chanongo.
Na Samira Said, DAR ES SALAAM
0 comments:
Post a Comment