Na Mwandishi Wetu
WILAYA ya Mkuranga imepanga kupeleka Mwenge wa uhuru katika kijiji cha wasanii kilichopo MWANZEGA, Mkuranga Julai 22, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii
Tanzania (SHIWATA), Cassim Taalib alisema jana kuwa mwenge utapokelewa
kutoka wilaya ya Rufiji katikia kijiji cha Kiparang’anda na baadaye
utakwenda moja kwa moja katika kijiji cha wasanii na wanamichezo cha
Mwanzega ambako utawasili saa 7 mchana.
Alisema kutokana na ujio wa ugeni
huo mkubwa SHIWATA imetangaza ofa ya siku kumi ambapo itapokea wanachama
kwa punguzo la asilimia 50 na kugawa bure viwanja vya kujenga nyumba
wasanii na wanamichezo ambao watapata nafasi ya kwenda katika sherehe na
watakabidhiwa viwanja vyao.
Wasanii na wanamichezo zaidi ya
600 wanatarajiwa kuondoka makao makuu ya shiwata ilala bungoni saa 12
asubuhi Jumanne asubuhi kwenda mkuranga.
Katika sherehe hizo kiongozi wa
mbio za Mwenge, ataweka jiwe la msingi katika kijiji cha wasanii
kuzindua rasmi kijiji hicho ambacho kinatarajiwa kuwekwa umeme, barabara
na miundombinu ya kisasa.
Taalib alisema katika sherehe hizo
msanii maarufu wa atavishwa joho ya kutawazwa kuwa balozi wa kwanza wa
kijiji cha wasanii na wanamichezo hapa nchini.
SHIWATA pia inatoa pongezi kwa
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mkuu wa Mkoa wa Pwani,
Mkuuu wa Wilaya ya Mkuranga, Viongozi wa Tarafa ya Shungubweni kata ya
Mbezi,viongozi wa Mwanzega,Ngarambe.
Alisema kutakuwa na mkutano wa wasanii
0 comments:
Post a Comment