Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa washukiwa wa matukio ya tindikali visiwani hapa Alawi Mohammed Silima (25) mkazi wa Fuoni Melinne nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta
Mohammed Mhina, amesema mtuhumiwa anahusishwa na tukio la kumwagia
tindikali Sheha wa Shehia ya Tomondo mjini Zanzibar Bw. Mohammed Omar
Saiidi Kidevu kabla ya kutoweka.
Inspekta Mhina amesema, Mtuhumiwa huyo ambaye kwa muda mrefu
alikuwa akisakwa na Polisi kwa kuhusina na tukio hilo, alikamatwa juzi
usiku akiwa mafichoni katika enero Fuoni baada ya taarifa za
kiintelijensia kubaini kuwepo kwake.
Bado Makachero hao wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo kwa lengo
la kuubaini mtandao mzima wa matukio mbalimbali yakiwemo ya tindikali
yaliyotokea siku za nyuma visiwani humo.
Kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na taarifa za siri za
raia wema ambapo Jeshi la Polisi lilikua likiendelea na upelelezi wa
chini kwa chini wa kumbaini mtuhumiwa na mahali alipojificha.
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wamepongeza kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo na kuliomba Jeshi la Polisi kuendelea na juhudi zake za
kuwafsaka watuhumiwa wengine wanaohusika katika matukio menginne kama
hayo siku za nyuma viisiwani hapa.
Tukio la kumwagiwa tindikali kwa Sheha huyo, lilitokea majira ya
saa 2.45 usiku Mei 22, mwaka jana, wakati Sheha huyo alipokuwa akirudi
nyumba akitoka kuchota maji nyumba jirani. na kujeruhiwa vibaya
mgongoni, kifuani, sikio na jicho la upande wa kulia.
0 comments:
Post a Comment